Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Haya ndio yanayo tendeka kwenye Ofisi zetu

Mini-skirts have become a norm on dress down Friday as many people gear up for the night ahead and hit the town straight after work


Kumekuwa na kero mbalimbali pindi tunapoenda kwenye ofisi mbalimbali kupata huduma katika ofisi hizo na hizi ndizo sababu zinazofanya wafanya kazi wangi wasiwe makini na kazi walizopewa na waajiri wao.
     Ø  Mapenzi kazini;
Kiza hiki cha digital mapenzi yamekuwa wazi wazi na sio kificho tena kama wazee wetu wazani walikuwa wanafanya mambo yao kwa siri sana lakini hivi sasa vijana hawajali wapo wapi hata maofisini sasa wanatumia kufanya uchafu wao haijalishi ni mfanyakazi mwenzake au kutoka nje ya ofisi. Imefikia hatua wafanyakazi wanafanya mapenzi hata kwenye vyoo ya ofisi. Maofisini sasa kumekuwa hakuna amani tena maana haijaalishi ni mke/mume wa mtu wote wamekuwa ni wafuska tu.
 
Huko ndiko baadhi ya ndoa zimevunjika kutokana na kusalitiana wakiwa kazini. Ndio maana wanaume wangine wanawaachisha kazi wake zao baada ya kuona mienendo ya wake zao kuwa mibaya. Na baadhi ya maboss wa siku hizi wamekuwa na tamaa sana kutembea na wafanyakazi wake kwa kuwa ahidi kuwaongeza mshara au kuwapandisha cheo. Imekuwa kitu cha kawaida kwa wasichana kutoa rushwa ya ngono ili kupata kazi kwa sasa kazi zimekuwa ngumu sana na isitoshe kuna wanafunzi wengi ambao wanamaliza elimu ya juu na kutegemea kuajiriwa.

Images

Nini madhara ya kupenda kupita kiasi..


Female finches forced to take an inferior husband display high stress levels... just as it is in the human world


Kupenda ni jambo muhimu katika maisha ya mwanadamu, kwa sababu asilimia kubwa ya matendo ya mtu huongozwa na mapenzi. Miongoni mwetu kuna watu wanapenda
waume/wake zao, mali, watoto, magari vyakula,vinywaji, michezo na pengine aina fulani ya maisha.

Baadhi yetu tuko tayari kupoteza maisha kama tutaachwa na wapenzi au kukosa mambo tuliyoyapenda. Pamoja na kwamba moyo hupata maumivu pale mazuri yanapokosekana, bado kuna ukweli juu ya madhara ya kujitakia yanayoweza kuepukwa na mtu anayeumia kwa kiwango cha kukosa usinginzi, kulia mara kwa mara kiasi cha kushindwa kufanya kazi zake kama kawaida.

Kupenda kwa kiwango cha kushindwa kujizuia na kuvumilia ni hatari kwa afya ya mwanadamu, kwani uchunguzi unaonesha kuwa watu wengi wanaosumbuliwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo,moyo na wale wenye magonjwa yasiyoonekana kitalaamu pamoja na wanaokufa ghafla ni athari za msongo wa mawazo utokanao na kukosa mazuri wanayohitaji katika maisha yao.(Jiulize ni kipi kinachokutia simanzi moyoni mwako).

Images

Tambua siku za hatari kupata Mimba

Alexandra Kinova, 23, gave birth to four sons and a daughter by Caesarean section today

Mada yangu leo inahusu siku za hatari ambazo mwanamke akifanya ngono bila kinga basi anakuwa katika hatari ya kushika mimba.

Nimeamua kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya utoaji mimba, utupaji wa watoto  na hata kuwa na watoto wa mitaani yanasababishwa  zaidi na mimba ambazo hazikutarajiwa ambazo zingine zinatokana na mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga.

Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko hiyo iko katika makundi makuu matatu3 ambayo ni : mzunguko mfupi(siku25 kurudi nyuma), mzunguko wa kawaida(siku28) na mzunguko mrefu(siku30-35)

 Wanawake wengi mzunguko wao  huwa  ni wa kawaida yaani siku 28 hawa ndio leo nitawaongelea zaidi.

Images

Jifunze jinsi ya kuandika Mradi



Andiko la Mradi ni maelezo yanayoelezea mradi husika kwa kujibu maswali ya vihatarishi vya mradi, fursa zilizopo, rasilimali na jinsi vitakavyotumika, mpangilio mzima wa kuutekeleza mradi ikiwa ni pamoja na uongozi na usimamizi, mpango endelevu wa mradi kwa hapo baadaye kwa upande wa kitaasisi na kifedha
1.         Mradi huo unaitwaje?, Utakuwa maeneo gani?, Unafanyika kwa muda gani?, bajeti yake ni kiasi gani?, Wafadhili wa mradi ni akina nani?, Namba ya mradi kama ipo na kipindi cha kuanza na kumalizika kwa mradi.
2.         Maswali mengine ni kama ifuatavyo; Historia ya tatizo lililo sababisha mradi kuwepo ni ipi?, Mradi huu umetokana na serikali, mtu mmoja au jamii na ulianzaje au wazo lilianza nkwa nani?
3.         Kwanini tuwe na mradi huu katika jamii hii kipindi hiki?, Je, mradi ni suluhisho halisi na sahihi la tatizo hilo?, Je unadhani kama hautatekelezwa kwa sasa mradi huu utaleta madhara yoyote? Kuna ulazima wowote wa kuufadhili mradi huu?
4.         Unaweza kusema kwa ufupi mradi huu hasa unashughuli zipi na unatekelezwaje katika jamii hii.
5.         Utasimamiwa na nani au watu wangapi na kwa nafasi zipi kwa njia gani hasa ili kuwafikia jamii?, Je mradi huu utahusisha watu wangapi kiutendaji na pia utawalenga watu kiasi gani na wanawake wangapi na waume wangapi?

Images

Hatua (5) za kuongeza tija kwenye kazi

Business people working together in an office


Natumaini utakuwa mwenye nguvu, afya njema na mchangamfu, leo nataka nikujuzi mambo haya yatakayo kuongezea  tija katika kazi zako na maisha yako kiujumla. Kanuni moja na nzuri ya  kuongeza tija katika kufanikisha au kupata matokeo makubwa ni hii

  Kanuni hiyo itakusaidia kusonga mbele kimaendeleo na kuongeza ufanisi wa kazi zako, kuwa na faraja kwa kitu unachofanya huchochea uwajibikaji na uhodari wa utendaji wako kazi. Ndio maana kujua nini unapenda kufanya ni muhimu sana kwenye mafanikio kwa kuwa faraja hutia mbolea ya matumaini na hukupelekea wewe kutaka kutenda mambo makubwa zaidi na mazuri katika kazi unayoifanya.

Zingatia mambo haya, 
1. Kuwa na sababu nyingi za kutopata mafanikio kutakufanya ukwame na kudumaza utendaji    wa     kazi zako. Epuka kuwa na visingizio vingi vya kutokuwa mtendaji mzuri wa kazi zako.
2. Huwezi pata matokeo mapya na mazuri ikiwa utaendelea kufanya maamuuzi  ya zamani. Kila siku kuwa na mawazo mapya na mbinu mpya za kukujenga na kuongeza ufahamu wako wa kazi unayoifanya.

Images

Mashart 5 katika kupata mkopo Benki





Masharti Tano (5) Muhimu Katika Kupata Mkopo wa Benki?
1.       Je ni biashara mpya au inayoendelea?
Biashara inayoendelea na yenye angalau miaka mitatu ina nafasi kubwa kuliko zile changa au mpya
2.       Aina ya biashara unayofanya
Biashara za kuzalisha zinanafasi kubwa kuliko zile za huduma au uchuuzi
3.       Integrity (historia safi )ya mkopaji
Historia safi ya mkopaji ya kukopa na kurudisha bila usumbufu inaongeza uwezekano mkubwa wa kupewa mkopo
4.       Dhamana na mdhamini wa mkopaji kama akishindwa kurudisha
Kwa bahati mbaya mkopaji akishindwa kurudisha kwa namna yeyote ile mkopo, je kitu gani kitafidia huo mkopo ili benki wasipate hasara AU nani atasimama kama mdhamini ili yeye ndie ashikwe endapo mkopaji atashindwa kurudisha mkopo. Aina ya dhamana na mdhamini atakayekubaliwa na benki itasaidia wewe kupata mkopo