Mabusha ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa
korodani. Hali hii hutokea kunapokuwa na mkusanyiko wa maji kati ya tabaka
mbili za utando unaozunguka korodani.
Inakadiriwa kuwa karibu asilimia moja ya wanaume
wote kote duniani huathiriwa na tatizo hili. Kwa hapa nchini, tatizo hili ni
maarufu sana maeneo ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kiasi cha
kuhusishwa na imani kadhaa.
Mabusha
husababishwa na nini?
Sababu za kutokea kwa mabusha hutofautiana kati ya
watoto wa kiume na wanaume watu wazima.
Kwa
watoto wa kiume, mabusha huweza kuanza kutokea kipindi
cha ujauzito. Wakati wa ujauzito, korodani za mtoto wa kiume huwa kwenye tumbo
lake kabla ya kushuka taratibu kuelekea kwenye mapumbu. Wakati wa ushukaji huo,
kifuko kinachozunguka korodani kinachoitwa processus vaginalis hushuka sambamba
na kurodani hizo na kufanya korodani kuzungukwa na maji.
Kwa
wanaume watu wazima, mabusha husababishwa na mambo makuu
mawili; Kwanza, kitendo chochote kinachochochea tando zinazozunguka korodani
kuzalisha maji kwa wingi kuliko kawaida, na njia ya pili ni kupungua kwa
ufyonzaji wa maji yanayozunguka korodani kwa sababu ya kuziba kwa mirija ya
lymph (blockage of scrotal lymphatic system) au kuziba kwa mishipa ya damu
inayosafirisha damu kutoka kwenye pumbu kwenda sehemu nyingine za mwili
(blockage of scrotal venous system).
Ongezeko
la uzalishaji wa maji linaweza kutokana na
• Maambukizi
au/na majeraha katika korodani (testicular inflammation au orchitis) au
maambukizi katika mshipa ujulikanao kama epididymis yanayoweza kusababishwa na
kifua kikuu (tuberculosis) cha makende, au maambukizi yanayosababishwa na
vimelea wa filaria (filariasis) wanaosababishwa na kuumwa na mbu aina ya Culex.
• Kujinyonga
kwa korodani (testicular torsion) kunakoweza kuzifanya korodani kutenda kazi
zaidi ya kiwango chake (hyperactive testis).
• Uvimbe
katika korodani (testicular tumors) ambao husababisha uzalishaji wa maji kupita
kiasi.
Kupungua kwa ufyonzaji wa maji hutokana na
• Kufanyiwa
upasuaji kipindi cha siku za nyuma katika eneo la kinena, au operesheni ya
upandikizaji figo ambazo zinaweza kuathiri mfumo wa lymph na vena na hivyo
kupunguza ufyonzaji wa maji kutoka kwenye mapumbu.
• Kuwahi
kufanyiwa tiba ya mionzi kipindi cha nyuma nayo uhusishwa na kutokea kwa
mabusha.
Kwa hapa kwetu Tanzania, kung’atwa na mbu aina ya
Culex anayeeneza vimelea vya filaria kunaelezwa kuwa sababu kuu mojawapo
inayopelekea kuwepo kwa tatizo la mabusha na matende hususani maeneo ya Pwani
na mwambao.
Dalili
za Mabusha
Katika hatua za awali, mabusha hayana dalili zozote
(asymptomatic).
Hata hivyo, baada ya muda fulani, mapumbu hujaa na
uvimbe huweza kuonekana hata kwa nje. Kwa kadiri uvimbe unavyozidi kuongezeka,
dalili zifuatazo zaweza kujitokeza pia;
• Muhusika
kujihisi hali ya uzito na kuvuta sehemu za siri kutokana na kujaa na kuongezeka
kwa uzito wa mapumbu.
• Mgonjwa
huweza kujihisi hali ya usumbufu na kutojisikia vizuri maeneo ya kinena mpaka
mgongoni.
• Kwa
kawaida mabusha hayana maumivu yeyote. Hata hivyo, iwapo mgonjwa ataanza
kujihisi maumivu, hiyo ni dalili ya kuwepo kwa uambukizi katika mshipa wa
epididymis (acute epididymitis)
• Uvimbe
huwa na tabia ya kupungua iwapo mgonjwa atakaa kitako na huongezeka pindi
anaposimama.
• Iwapo
mgonjwa atajisikia homa, kichefuchefu na kutapika, hizo ni dalili za kuwepo kwa
uambukizi katika mabusha.
• Kwa
kawaida mabusha hayana muingiliano na uwezo na ufanisi wa utendaji wa ngono.
Hata hivyo kuna taarifa tofauti za kitafiti kutoka bara Asia na Afrika
Magharibi kuwa mabusha yanaweza kuathiri ufanisi wa ngono na kwa kiasi fulani
kusababisha mhemko au msongo wa mawazo kwa muathirika.
Uchunguzi
na Vipimo
Uchunguzi mzuri wa kitabibu (physical examination)
huwezesha kugundua uwepo wa mabusha kwa kiasi kikubwa bila hata kuhitaji vipimo
vya ziada. Vipimo uhitajika tu kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha mabusha,
madhara yaliyoletwa na mabusha au kujua hali ya korodani.
Vipimo
ni pamoja na
• Kupima
damu (Full Blood Count) na mkojo (Urine Analysis) kuchunguza uwepo wa
maambukizi kama vile vimelea wa filaria na mengineyo.
• Ultrasound
ya kinena pamoja na mapumbu: Aina hii ya kipimo hufanywa ili kuchunguza uwepo
wa matatizo mengine tofauti na mabusha. Matatizo hayo ni kama vile ngiri,
uvimbe, kujinyonga kwa korodani (testicular torsion), majeraha katika korodani,
damu kuvuja kwenye kwenye korodani (traumatic hemorrhage) au maambukizi.
Matibabu
ya Mabusha
Kwa watoto wadogo, kwa kawaida mabusha hupotea
yenyewe ndani ya mwaka mmoja. Iwapo hayajapotea, mtoto uhitaji kufanyiwa
upasuaji kama tiba.
Kwa wanaume watu wazima, mabusha pia huweza kupona
yenyewe bila kuhitaji tiba. Iwapo mabusha hayajapotea na yanamletea mgonjwa
usumbufu (discomfort) au hali mbaya ya kiumbo (disfigurement) hayana budi
kufanyiwa upasuaji ili kuyaondoa.
Njia
za tiba ni
• Upasuaji:
Upasuaji wa mabusha huweza kufanyika bila ya mgonjwa kuhitaji kulazwa
(outpatient). Madhara yanayoweza kutokea wakati wa upasuaji wa mabusha ni
pamoja na damu kuganda (blood clots), maambukizi au majeraha kwenye korodani.
Hii ndiyo njia maarufu zaidi na ya kuaminika ya matibabu ya mabusha duniani
kote.
• Kunyonya
maji kwa kutumia sindano maalum (Needle aspiration): Njia nyingine inayotumika
kutibu mabusha ni kuyanyonya maji kwa kutumia sindano maalum (needle
aspiration). Hata hivyo njia hii haitumiki sana sehemu nyingi duniani kwa sasa
kwa sababu maji ya mabusha huwa yana tabia ya kujirudia baada ya muda mfupi
hata kama yatanyonywa.
Baadhi ya matabibu hupendelea kudunga dawa maalum za
kuzuia maji yasijae tena (sclerosing agents) mara baada ya kunyonya na
kuyaondoa maji yote.
Njia hii ya kunyonya maji ya mabusha, hufaa zaidi
kwa wagonjwa wasioweza kuhimili upasuaji. Madhara yanayoweza kusababishwa na
tiba ya namna hii ni pamoja na maambukizi na maumivu kwenye korodani.
Hata hivyo wakati mwingine, bila kujali ni tiba gani
imetumika, mabusha huweza kujirudia baada ya matibabu.
Madhara
ya Mabusha
Kwa kawaida mabusha hayana madhara yeyote. Aidha
mabusha hayawezi kuathiri uwezo wa mtu kuzaa. Hata hivyo mabusha yanaweza
kuleta madhara iwapo tu kama yakiambatana na magonjwa mengine kwenye korodani.
Kwa mfano, kama mabusha yataambatana na maambukizi
(testicular infection) au uvimbe kwenye korodani (testicular tumor), yanaweza
kusababisha kupungua kwa uzalishaji na utendaji kazi wa mbegu za kiume (sperms)
na kupelekea tatizo la ugumba kwa wanaume.
Hali
kadhalika, iwapo sehemu ya utumbo mkubwa au mdogo imebanwa
katika upenyo fulani kwenye sehemu ya ukuta wa tumbo, huweza kusababisha ngiri
(strangulated hernia), hali ambayo ni hatari kama isipotibiwa haraka
0 comments: