WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725
BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725
MPENZI ANAYEKUPENDA KWA DHATI ATAKULINDA HAHALI POPOTE...!!!!! SOMA HAPA
Penda
Kujiona Mtu Nambari Moja Kwa Ubora Kwa Sababu Mungu Aliona Una Umuhimu Ndiyo
Maana Akakuumba. Linda Thamani Na Heshima Yako, Usikubali Mapenzi Yakuondolee
Nguvu Ambayo Mfalme Wa Mbingu Na Ardhi Amekupa. Ni Rahisi Kudharauliwa Ikiwa Utakuwa Na Mtu Ambaye Hana
Mapenzi Ya Dhati Na Wewe. Atakusaliti, Watu Watazungumza Pembeni. Atakusema
Vibaya, Ukipita Mitaani Utaonekana Kituko. Mpenzi Mwenye Uelewa Na Anayekupenda
Kwa Dhati, Atakulinda Mahali Popote.
Hatakusaliti, Ataishi Ndani Yako. Linalokuuma, Litamtesa. Wasiokupenda
Atawachukia. Marafiki Zako Atawageuza Ndugu. Kinyume Chake Ni Kwamba Mwenzi
Asiyekupenda Kwa Dhati, Si Ajabu Akashiriki Kukumaliza.
Kuna Watu Hawaoni Hili Umuhimu, Mpenzi Maana Yake Ni Msiri Wa Maisha Yako.
Unapokuwa Umelala Fofofo Hujitambui, Ubavuni Kwako Yupo Yeye. Anaweza Kukufanya
Lolote Wakati Wewe Unaogelea Ndotoni. Mpende Akupendaye Mapenzi Ni Hisia.
Ni Rahisi Kwako Kujua Kwamba
Uliyenaye Anakupenda Kwa Dhati Mnapokuwa Mnazungumza. Je, Anakusikiliza Kiasi
Gani?
Mtu Ambaye Hana Mapenzi Na Wewe, Hata Umwambie Kwa Lugha Gani Hawezi Kukuelewa.
Tena Inawezekana Ulizungumza Naye Jana Kwa Herufi Kubwa, Lakini Leo Jua
Limechomoza Anarudia Yale Yale.
Inawezekana Ulimuonya Kuhusu Tabia Ambazo Zinakufanya Heshima Yake Ipotee.
Hakatazwi Kuwa Na Marafiki Wa Jinsia Nyingine, Lakini Mazoea Yake Siyo Mazuri
Kiasi Kwamba Wanaweza Kutembea Barabarani Wameshikana Viuno. Ikiwa Unamueleza
Habadiliki, Huyo Hakupendi.
0 comments: