Leo hii nitazungumzia
biashara ya kununua mahindi, kukoboa, kusaga na kuuza unga wa sembe kwa wateja.
Hii ni biashara nzuri sana kama utakuwa makini kwenye utekelazaji wake.
Leo tutazungumzia
upatikanaji wa mahindi na Mambo unayotakiwa kuangalia ni kama ifuatavyo:
Mtaji wa biashara
Hakikisha una mtaji wa
kutosha utakao wezesha kufanya yafuatayo:
-
Kulipia pango la sehemu ya
biashara
-
Kununua mahindi, kukoboa,
kusaga,kufunga kwenye mifuko
-
Kulipia gharama za
kusafirisha unga kutoka masjine hadi sehemu yako ya biashara
- Pesa ya kutosha kulipa
mishahara ya wafanyakazi angalau miezi mitatu ya mwanzo
- Akiba kwa ajiri ya dharura
Upatikanaji
wa mahindi
Lazima ufahamu kuwa
upatikanaji wa mahindi hutegemea msimu. Kuna wakati mahindi yanakuwa mengi
sokoni na bei yake inakuwa nafuu. Wakati ambao sio wa msimu mahindi yanakuwa
machache na bei yake ni ghali. Kwa wale wanaoishi Dar es Salaam hutegemea
mahindi kutoka Songea, Iringa, Mbeya, Rukwa na Dodoma
Msimu mzuri wa mahindi kwa
wafanya biashara wa Dar ni June – December na msimu mbaya ni January – Mei. Kwa
Dar es Salaam mahindi yanapatikana Manzese Darajani au Tandale asubuhi na
mapema kila siku ispokuwa Jumapili na sikukuu
Aina
ya Mahindi ya Kununua
Itabidi upate uzoefu wa
kufahamu aina nzuri ya mahindi kununua ambayo ni yale yenye kutoa unga mwingi
na pumba chache. Mahindi mabaya ni yale yenye kutoa pumba nyingi na unga
mchache. Kwa taarifa yako, mara nyingi mahindi yenye mbegu kubwa uhusishwa na
pumba nyingi, unga mchache
Jinsi
ya Kununua mahindi
Inategemea na ukubwa wa
mataji alionao mfanya biashara ambapo kama ana uwezo ni heli anunue mahindi
mengi kwa wakati mmoja na kuyaweka ili wakati bei ya mahindi ikipanda basi yeye
atakuwa hana matatizo
Kama nafasi ya
mfanyabiashara kipesa siyo kubwa sana anaweza akanunua mahindi ya gari zima;
yaani tani 10, 20 au 30 kutegemea uwezo wake kipesa.
Wengine hawana uwezo wa
kununua mahindi ya kujaza gari zima lakini wamo kwenye hiyo biashara.
Wanachofanya ni kuungana wafanyabishara wadogo watatu au wane na kuchanga pesa
za kuweza kununua gari zima
Upatikanaji Mashine ya
kukoboa na kusaga mahindi
Kama una mtaji wa kutosha
basi ningekushauri ununue mashine ya kukoboa mahindi na ya kusaga unga. Lakini
kwa kuwa unaanza hii biashara kwa mara ya kwanza sio vizuri kutumia pesa nying
kununua mashine wakati bado huna uhakika na biashara yenyewe.
Unachoweza kufanya ni
kukoboa mahindi na kusaga unga ukitumia mashine ambazo tayari zipo na gharama
yake huwa ni nafuu. Kwa wale wakazi wa Dar es Salaam juna mashine nyingi tu
maeneo ya Manzese Darajani na Tandale
Ufungaji wa unga kwenye
mifuko
Kwa wakazi wa Dar es Salaam
pale Tandale wako wataalamu wa kuchora nembo itakayotumika kutambua biashara
yako na vile vile watapiga chapa mifuko yako. Gharama huwa inakuwa juu kwa mara
ya kwanza lakini gharama hiyo upungua baadaye kwa kuwa utengezaji wa nembo
hufanyika mara ya kwanza tu.
Unaweza ukatengeneza mifuko
ya ujazo wa 5kg, 10kg, 25kg na 50kg kutemea na aina ya wateja utakaohudumia
Uuzaji unga wa sembe
Hii hatua inahitaji upate
msaada kutoka kwa washauri wa masoko (marketing consultants) ambao
watakuelekeza jinsi ya kufanya utafiti wa soko, kujitangaza, kutangaza bidhaa,
mikakati ya mauzo na kadhalika
Mahali pa kufanyia biashara
Hakikisha kuwa unapata
sehemu nzuri ya kufanya biashara ambapo kuna nafasi ya kutosha kufanya biashara
na pana vutia kwa wateja. Pia pawe na usalama wa kutosha kwa wateja na vifaa
vya kufanyia kazi
Aina ya wateja
utakaohudumia
Ni vizuri ufanye uamuzi ni
wateja gani unataka kuwahudumia- wafanyabiashara ya unga wadogo, kati au
wakubwa
Tafiti ni aina gani ya
huduma wateja wanapenda
Baada ya kufahamu aina ya wateja unaotaka
kuwahudumia ni vizuri kufahamu ni huduma gani inavutia hao wateja wako.
Weka vivutio sehemu ya
kufanyia biashara
Hakiksha sehemu ya biashara
inavutia kwa kuweka vifaa kama television, music system, air conditioner na
kadhalika
Mvuto wa Wafanyakazi
Hakikisha wafanyakazi
watakatoa huduma kwa wateja ni nadhifu na wanapendeza kutokana na mavazi yao.
Pia wafanyakazi wawe wachangamfu kwa wateja
Bei ya unga wako wa sembe
iwe yenye mvuto
Hakikisha bei za mifuko
yako ya unga sio za chini sana kiasi cha kufanya biashara iendeshwe kwa hasara
au za juu mno kufanya wateja washindwe kuzimudu
Uwekaji wa hesabu za biashara
Unatakiwa uwe na utaratibu wa kuweka kumbukumbu
za manunuzi ya vitu, malipo mbali mbali, pesa za mauzo na kadhalika. Kumbukumbu
hizo ndizo zitakazosaidia kutengeneaza hesabu zitakazoonyesha kama biashara
inaendeshwa kwa faida au hasara
Weka pesa zako benki
Hakikisha pesa zote
zinazotokana na biashara zinawekwa benki. Usichanganye pesa za biashara na
matumizi yako binafsi
Asante sana kwa kutuelimisha
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteVipi kuhusu swala la tbs mkuu
ReplyDeleteAsante sana kwa Ushauri mzuri wa kitalii, Ninahitaji mtengenezaji na mchapishaji wa Mifuko ya kuuzia Unga wa Kilo moja na Kilo mbili,anayemjua mchapishaji awasiliane na mm kwa no. 0754499242 au 0715499242
ReplyDeleteasante sana kwa fursa hii nzuri zaidi hasa kwa sisi vijana tunaotaka kujikwamua toka kwenye umasikini.
ReplyDeletenimependa elimu yako tatizo ni uatikanaji wa mitaji
ReplyDeleteasante kwa elimu ulionipa ndugu
ReplyDeleteSomo zuri sana... Natarajia kuanza hii biashara hivi karibuni, shukrani kwa wazo lako
ReplyDeleteAsante kwa elimu hii ,, but mimi naomba kujua bei ya mfuko tupu wa kilo 5 / 10 / 15 / 25/ 50 unauzwaje na inapaikana wapi
ReplyDeleteUkishapata nembo tako (logo) huwa zote ni bei moja 450 mpaka 510
DeleteAsante Sana. Hivi mashine ya kusaga na kukoboa inauzwaje? Naomba tathmini kwa anaefahamu.
ReplyDeleteno ushauri mzuri sana nashukuru kwa kuniamsha kwani tangu sasa nitaufuata ushauri wako
ReplyDeletetatizo ni ubora kuna mchaniaji hapo ameuliza swali zuri sana suala la TBS
ReplyDeleteAsante sana kwa somo zuri......
ReplyDeleteAsnte kwa Elimu nzuri.
ReplyDeleteTafadhali naomba msaada wa upatikanaji wa mifuko ya 1kg na 2kg.
Naomba niweze wasiliana na yeye kwenye namba 0714617742
Hio ni elimu bila ya mipaka, Ahsante kwa ushauri uliojaa elimu na mafunzo.
ReplyDeleteVijana wenzangu fursa ya elimu hii tuitumie ili tujikwamue kutoka kwenye giza la umasikini.
Ukitaka kufanya packing lazma uwe na certificate za tfda na tbs?
ReplyDeleteSafi sana ila Mimi nataka mtu anayeuza sembe kutoka Rukwa mamba yangu ni 0625529049 kwa being nzuri na Mimi nataka kuuza jumla
ReplyDeleteJe! Unatafuta mkopo kuanza biashara, kulipa bili yako, tunatoa mkopo wa $ 3,000 hadi $ 500,000,000.00, tunatoa au aina ya mkopo hapa na 2%. Ninatarajia sasisho lako kuhusu suala hili. Asante kwa muda wako na uelewa! Kwa hiyo kurudi kwetu ikiwa una nia .. Tafadhali wasiliana nasi kwenye barua pepe yetu: Fredjosephloans@gmail.com
ReplyDeleteelimu nzuri. wadau natafut marketing and sales officer tuwasilaie 0628099135
DeleteKama Kuna mtu anamiliki kampuni ya kutengeneza mifuko ya kupaki sembe anichek 0659461097(WhatsApp)
ReplyDeleteNimeipenda sana hii lakini vp kuhusu tbs
ReplyDeleteTbs ya nini sasa kwani unga wa ugali si unasagwa na mahindi au
DeleteAsante Sana naomba anayetengeneza mifuko ya 1kg na 2kg anitafute
ReplyDelete0687401069
Asante mkuu. Naomba kwa yeyote anayetengeza mifuko tuwasiliane kupitia 0744595434
ReplyDeleteMtaji kama shingapi kianzio mkuu
ReplyDeleteMtaji kama shingapi kianzio mkuu
ReplyDeleteKwa kweli umenifanya nifike mbali na kupata jibu ya mashine yangu ya kosaga na kukoboa naomba kupata namba ya mwenye logo pia Kwa ambaye tayari amekwisha Anza kusambaza ili kupata maujuzi ya biashara hiyo tuwasiliane Kwa no. 0754657844 or 0686657844 pls
ReplyDeleteNaomba anayejua ntakapoweza kupata mifuko awasiliane nami kwa namba 0659469874
ReplyDeleteHii blog ipo active kweliii
ReplyDelete