Madhara
yanayoambatana na utoaji mimba ni vifo, kupoteza damu nyingi, kifafa cha uzazi
na maambukizi hatarishi katika mfuko wa uzazi au mirija ya uzazi. Haya yote
yanaambatana na homa kali na maumivu makali, kutunga usaha kwenye kizazi na
kulazimika kufanyiwa upasuaji wa dharura au haraka kitaalamu; kikubwa mara
nyingi ni kifo.
Mhusika
kama akipona kutokana na athari ya kuichokonoa mimba visivyo au kwa nguvu sana,
wakati mwingine husababisha uharibifu wa mfuko wa uzazi na mirija yake, na
hubakiwa na makovu kwenye ile ngozi laini ya mfuko wa uzazi, ambayo
humsababishia maumivu makali anapokaribia siku zake za hedhi ama kuupoteza
mzunguuko wake. Hii ni kwa muda mrefu au milele. Kitaalamu wanaita ni kupoteza
heshima ya uzazi (quality of life).
Athari nyingine ni kufungwa kwa kizazi, kwamba mirija ya uzazi ikijifunga basi mwanamke huyo hawezi tena kuzaa maishani mwake. Kutokana na kujifunga kwa mirija ya uzazi, athari ni kuwa mbegu ya yai la mwanaume ambayo ni ndogo hujipenyeza na kuingia, na mbegu ya yai la mwanamke ambayo ni kubwa hupita na yanapokutana kusabibisha mimba kutunga nje ya kizazi, ambayo kitaalamu huitwa “ectopic pregnancy”.
Kwa kuwa mimba hiyo iko nje ya mazingira ya kawaida, inaweza ikapasuka na kupoteza damu nyingi na kusababisha kifo na ikiwahiwa ni kufanyiwa upasuaji na kulifunga eneo hilo.
Athari nyingine ni ugumba ambao kitaalamu unajulikana kama “infertility”. Hali hii inatokana na uharibifu wa mazingira ya mpango wa mfuko wa uzazi na hasa kwa uchokonoaji wa mimba, hivyo kufungwa kwa kizazi, pengine hedhi inakoma na kwa kutopata hedhi wanawake wengi huchanganyikiwa.
Tatizo hili la ugumba huwa linasababishwa na kukwanguliwa kwa ile ngozi laini inayozunguka tumbo la uzazi. Kukwanguliwa huko kunatokana na ama vifaa vinavyotumiwa kuichokonoa mimba hiyo au madawa makali.
Athari nyingine kama uchokonoaji umepita kiasi na kufikia kwenye utumbo mkubwa huathirika na kusababisha utumbo kutobolewa na kuwekwa mrija wa kutolea choo kikubwa.
Vile vile hali hiyo usababisha ugandaji wa damu kwenye mishipa ya fahamu kuelekea kwenye ubongo. Hii ni hatari mno, kwani inasababisha mhusika kuwa na hali kama ya kiharusi.
Kutokana na athari hizo na hasa ugumba, wanawake hupatwa na msongo mzito wa mawazo na kuchanganyikiwa kisaikolojia, hivyo huanza kuwa na tabia za ajabu za hasira na hata chuki kwa wenzao wenye watoto na hata kuwachukia watoto wa wenzao pasipo sababu za msingi. Wanajihisi wamekosa ule ubora wa kuitwa mwanamke.
Hapa nchini, sheria inayoruhusu kutoa mimba haipo, hivyo jambo hili ni kosa na hivyo hufanywa kwa kificho, pengine katika mazingira yasiyofaa, kukosa ujuzi wa kitaalamu na vifaa visivyo sahihi. Wakati mwingine ni wasichana wenyewe hushawishiana jinsi ya kutoa mimba na kusasabisha madhara yote haya.
Baadhi ya wasichana baada ya kukumbwa na tatizo la ugumba hujifariji kuwa ati wamebaki na uzuri wao na hapo hujiingiza kwenye biashara haramu ya kuuza miili yao na kujiweka kwenye hatari ya maambukizi ya magonjwa ya ngono na kupata ukimwi pia.
Kutoa mimba huleta ulemavu wa maisha, kutokuzaa kabisa na ni kifo. Natoa rai kwa wanawake wote waachane na tabia hiyo ya kuzichokonoa mamba, na waachane na kubeba mimba wasizozipanga, pia waepuke tamaa za maisha ya starehe kwani zinawatumbukiza kwenye majanga.

0 comments: