Serikali leo imepiga marufuku kwa mawakala wa
kutafutia watu kazi kwenye kampuni mbalimbali, kisa ni kutia hasara serikali na
kuwa nyonya waajiriwa kwa makato makubwa yanayoenda kwa mawakala hao na
kumuachia muajiriwa hela ya mboga tu.
Kazi kupata mpaka uwe na mtu unaemfahamu
akufanyie mipango au utoe rushwa kwa waajiri katika ofisi wanao toa kazi.
Ona msululu wa watu hao wanagombania nafasi 1
ya kazi iliyotangazwa. Kazi zimekuwa
ngumu sana kupatikana, wasomi wamekuwa wengi wanao maliza Elimu ya juu tofauti
na zamani walikuwa wachache na nafasi za kazi zilikuwa nyingi kutokana na
uchache wa watafutaji wa kazi.
Ila sasa kila nyumba ina kijana aliyemaliza
chuo na yupo tu mtaani anatafuta kazi kama sio hivyo basi kuna mwanafunzi bado
anasoma chuo. Ajira hapa nchini kwetu limekuwa ni janga la kitaifa kila mtu
anataka kuajiriwa.
Wanasahau kwamba serikali haiwezi kuwapa
ajira wahitimu wote wa vyuo vikuu hapa nchini kwani ofisi ni chache kulingana
na idadi ya wahitimu kila mwaka kwa hiyo vijana wanashauriwa kujiajiri wenyewe.
Kuna fursa nyingi za vijana kujiajiri na
kuondokana kusubiri serikali ndio iwaajiri na hizi ni baadhi ya fursa vijana
wanatakiwa kuzitazama mara mbili mbili na kuzifanyia kazi; Ufugaji wa kuku,
Kilimo cha biashara, Stastionary, Printing T shirt, Kuuza matunda, Duka nk..
0 comments: