1. Utangulizi
A: Usajili
Kila mfanyabiashara wa
mazao ya misitu na nyuki anatakiwa na sheria kujisajili katika ofisi za meneja
misitu wilaya wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania au ofisi nyingine za
misitu zilizoteuliwa kutoa hati hizo. Ada za usajili kwa shughuli mbalimbali
zimetajwa katika sheria ya misitu Na. 14 ya 2002.
B: Leseni
Kila mfanyabiashara
anayetaka kuvuna mazao ya misitu sharti awe na leseni. Leseni zinapatikana
katika ofisi za misitu wilaya, mashamba ya miti au maafisa misitu walioteuliwa
na Wakala kutoa leseni hizo katika maeneo mbalimbali ya uvunaji. Wakala wa
Huduma za Misitu na Nyuki hutoa aina za leseni zifuatazo:
- Leseni ya uvunaji wa miti,magogo na nguzo – FD1
- Leseni ya kukusanya kuni kwa muda – FD2
- Leseni ya kukusanya mkaa na kuni kwa wingi – FD3
C: Alama ya nyundo
Kabla ya kutoa mbao, magogo
na nguzo ndani yam situ sharti zigongwe nyundo ya wakala wa huduma za misitu.
Nyundo hugongwa na maafisa misitu wanaosimamia maeneo ya uvunaji. Ina alama ya
FD na namba.
Hati ya kusafirisha mazao
ya misitu Transiti Pass (T.P)
- Baada ya mbao, magogo na nguzo kuhalalishwa kwa nyundo na kuhakiki uhalali na ujazo, hati ya kusafirisha mazao hayo yaani trasit Pass (T.P) hutolewa na maafisa misitu walioteuliwa.
- Pia mkaa,kuni na mazao mengine ya misitu yanayotoka nje ya wilaya husafirishwa kwa transit pass. Hakuna hati/kibali kinachotakiwa kwa kuni na mkaa unaosafiriswa ndani ya wilaya.
- Kila mkoa una majina ya maafisa walioteuliwa na wiazra ya maliasili na utalii kutoa kibali cha kusafirishia mazao ya misitu.
Hati ya kusafirisha mazo ya
misitu sharti zioneshe yafuatayo:
- Leseni ya kuvuna na stakabadhi ya malipo
- Jina la anayesafirisha mazao
- Aina ya miti
- Saizi na idadi/ wingi wa mazao
- Ujazo au uzito
- Aina na namba ya chombo kinachosafirisha mazao hayo
- Mahali yalikotoka na yanapopelekwa
- Majina ya vituo vya ukaguzi mazao yatakapopita
- Jina, cheo na sahii ya afisa anayetoa kibali
- Tarehe ya kutoa na kwisha muda wa kibali
- Jina na muhuri wa ofisi iliyotoa kibali
Mwenye mali anatakiwa
kusimama kwenye vituo vya ukaguzi wa mazao ya misitu ili akaguliwe.
E: Vitabu vya mali (Forest
Produce Stock Register)
Wafanyabiashara wote
waliyosajiliwa wanatakiwa na sheria kutunza vitabu vinavyoonesha rekodi za
mazao ya misitu yaliyopokelewa/ yaliyouzwa na nyaraka zinazohusika. Vitabu hivi
hukaguliwa mara kwa mara na maafisa misitu.
0 comments: