Hapa ninazungumzia kada ya wafanya biashara ambao mitaji yao haizidi TZS 5.0 million, ambayo mara nyingi huweza kuajili watu wasiozidi wanne na iwapo itatokea akafanya biashara mzunguko wake wa mauzo hauzidi TZS 12.0 million.
Mfano wa biashara zinazoangukia kwenye kada hii ni Ufugaji wa kuku, Mama Lishe, Useremala, Machinga, Wauzaji wa magenge na nyingine nyingi. Ni ukweli usio pingika kuwa jamii hii ya wajasiriamali wadogo pamoja na wale wa kati wanatoa mchango mkubwa katika mikakati ya Serikali ya kukuza uchumi na kupunguza Umaskini (MKUKUTA) kwa Tanzania Bara na Mpango wa Kukuza Uchumi Zanzibar (MKUZA).
Kwa kuelewa umuhimu huu, blog ya Siri ya Mafanikio imeamua kutoa elimu kwa ufupi kuhusu ujasiriamali mahususi kwa wafanya biashara wadogo wadogo sana (Micro businesses) ili kuwawezesha kutambua mbinu mbalimbali za kukuza, kuimarisha na kudumu katika biashara.
Kumbukumbu zimeonyesha kuwa sekta ya
Ujasiriamali kwa ujumla wake imechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi kama ifuatavyo:
- Kuongeza kipato na Ajira: hususan kipindi hiki ambacho kuna uhaba wa ajira za maofisini; watu wamekuwa wanajiajiri wenyewe kwa kuanzisha biashara ndogo ndogo kama tnavyoshuhudia utitiri wa vibanda vya mawakala wa M-pesa, Tigo Pesa, ‘stationary', maduka ya chakula n.k
- Ni chanzo kikuu cha bidhaa na huduma mbalimbali: Mifano ni bidhaa za chakula, uchongaji n.k
- Imechangia 50% ya Pato la Taifa
- Imechangia kuongezeka kwa idadi ya wajasiriamali.
0 comments: