1.
Ni
mtu anayekerwa na hali ilivyo(uncomfortable with status
quo) na yupo tayari kuwekeza muda,akili na nguvu zake ,pamoja
na rasilimali chache zingine alizonazo, kujaribu kuibadilisha.
2.
Anafahamu ni
kazi kubwa kubadili hali ilivyo sasa lakini,yupo tayari kukabiliana na
vikwazo ili kufikia lengo lake(ready to pay the price).
3.
Ni
mvumilivu, anayetambua fika kwamba Roma
haikujengwa siku moja,na
hivyo yupo tayari kupiga hatua moja baada ya
nyingine kuelekea lengo lake,bila kujali muda atakaotumia.
4.
Mwepesi wa
kujifunza mambo mapya(open minded),teknolojia na
utaalamu mpya,bila kujali ufahamu wake wa
awali.(anayetambua kwamba ukweli wa jana si
lazima uwe ukweli wa leo).
5.
Ni
mtu ambaye anatambua kwamba si lazima kuwa na
taarifa zote,[labda vile
vile kuwa na utaalamu wote na
hata mtaji wote] kuhusu jambo/biashara anayotaka kuifanya(ukweli ni
kwamba, mara nyingi hatuna taarifa za kutosha au
taarifa za kweli na anayeamini na
kutii zaidi msukumo kutoka ndani yake mwenyewe(internal
force).
6.
Anayefahamu ukweli kwamba hakuna kushindwa,
badala yake kuna mambo
ya kujifunza hususan wakati mambo hayaendi kama
tulivyotarajia.
7.
Anatambua kwamba anapoamua kufanya jambo lake,
labda kujaribu wazo lake la biashara,hana ulazima wa
kupata ruhusa ya
mtu yeyote,isipokuwa kutoka kwake mwenyewe.
8.
Ni
mtu anayeamini anaweza hata kama ndugu, majirani na
rafiki zake wana mtazamo tofauti kuhusu yeye.
9.
Ni mtu anayeonekana wa
kawaida,aliyeamua kufanya mambo yasiyo ya kawaida(An ordinary
determined to doing extraordinary staff)
10.
Ni
mwanamasoko(si lazima kwa taaluma)
bali kwa fikra zake,kwasababu hatimaye lazima bidhaa/wazo zifike/lifike sokoni.Ndio
wajasiriamali wote lazima wawe wanamasoko[All
entrepreneurs ought to be marketers].
0 comments: