Kama mfanyabiashara unaweza kutoka kwa kishindo sana kwa kuanza ukiwa huna kitu na kufanya kazi kwa juhudi sana ukiwa upande wa huduma(services) na kufanikiwa kutengeneza faida kubwa na kutokea hapo na kuanza kufikiria kuanza kukodi ofisi yako,kuajiri watu wengine nk ,ingawa ni rahisi kutoka ukiwa upande wa huduma lakini inahitaji ujuzi au weledi Fulani hivi ili uweze fika kilele cha mafanikio hapa simaanishi lazima uwe umesoma chuo kikuu maana ujuzi au utaalamu wa jambo halihusiani na degree ya chuo kikuu.
Unaweza
pata ujuzi kwa kuhudhuria semina mbalimbali,workshop mbalimbali,au kufundishwa
na mtu wenye ujuzi husika na baada ya kupata ujuzi kuanza fanyia kazi katika
maisha yako ya kawaida kila siku na kuwa bora kwa upande huo.
Nimejaribu
kuorodhesha aina zaidi ya 14 unaweza anzisha pasipo kuwa na mtaji kabisa au mtaji kidogo sana. Zifuatazo
ni baadhi ya biashara unazoweza anzisha kwa mtaji mdogo sana au pasipo mtaji
kabisa:
i.
Huduma za kuandika miradi
biashara(business plan),kama ilivyo kwa tafiti za uchanganuzi yakinifu(hali
halisi ya biashara)wajasiriamali wengi huwa huepuka kufanya kazi hii ngumu ya
kuandika mradi biashara(business plan) yao.Ukweli ni kuwa wajasiriamali wengi
hawajui hata kuandika business plan katika uwezo wa kuwashawishi wawekezaji
kuja kuwekeza na huwa hawawekezi muda wa kutosha kujifunza kwa hilo.Kama unaweza
timiza hitaji hili biasharaipomikononikwako.
ii.
Mshauri wa mambo ya biashara:Wewe ni
unauzoefu wa ujasiriamali au mmliki wa biashara?Unajua nini kinahitajika ili
uanzishe biashara,kujenga biashara,kuingoza biashara na kukua?Sasa unaweza
kuanza kazi ya ushauri wa biashara.Unaweza saidia kampuni au biashara
mbalimbali kutoka chini ya uvungu na kwa kutoa ushauri na maelekezo
muhimu.Unaweza kuwasaidi watu walioajiriwa kuanza kutoka kwenye ajira na
kuingia kwa ujasiriamali kwa malipo.
iii.
Huduma za kuandaa vitabu vya mahesabu.Wewe
ni mzuri katika kuandaa vitabu vya uhasibu vya kampuni au biashara
mbalimbali?unaweza weka ulingano kwa vitabu kwa vya uhasibu(hili ni jambo huwa
na shauku kulipata)? Sasa hamna kitu kinaweza kukuzuia wewe kuanza huduma za
kuandaa vitabu vya mahesabu anza sasa.
iv.
Kutoa huduma ya kuandaa nakuendesha
matukio(Event management),kampuni nyingi kila mara huwa na matukio
mbalimbali mfano semina,siku ya familia,sherehe mbalimbali mara nyingi kampuni
kama kampuni haiwezi kufanikisha kwa ufanisi uandaaji wa matukio haya,na hivi
ndivyo ilivyo kutokana na wafanyakazi wao kuwa na majukumu husika tofauti na
kuandaa matukio ya kampuni na kuyasimamia,hivyo ili kuwa na ufanisi hapa
inabidi kampuni zikodi watu wan je wenye ujuzi wa kuandaa shughuli husika kwa
uhakika,wewe kama una ujuzi na uzoefu wa kuandaa shughuli kama hizo mwanzo mpaka mwisho uwanja
ni wako.Mfano kuna matukio kama siku ya familia,semina kwa
wafanyakazi,maonyesho ya biashara ndani nan je ya nchi kwa kampuni husika
v.
Kuanzisha tovuti kwa huduma mbalimbali,Kwa
afrika watu kunufaika na tovuti ndio kwanza ipo steji za mwanzoni,Unaweza
anzisha tovuti na kutoa huduma ya taarifa watu wanatafuta ,baada kuwa mmiminiko
wa watu wengi wanaotembelea tovuti yako,unaweza sasa ongea na kampuni kadhaa
kuja kutangaza na wewe na kutengeneza
fedha za kutosha.Kama hujui jinsi ya kutengeneza tovuti usijali kuna tovuti za
bure kabisa ambazo zimetengenezwa tayari
kinachohitajika ni wewe kujaza fomu zao na ndani ya dakika moja unakuwa na wewe tovuti yako,na kama unahitaji nunua
domain unaweza ikawa moja kwa moja tovuti yako.
vi.
Mshauri wa masoko,Je wewe unaweza
nionyesha mimi njia ya gharama ndogo ya kuongeza wateja wangu kuanzia aslimia 30% -70% au zaidi?kama ndio biashara
ipo mikononi mwako.Unaweza jiweka wewe mwenyewe katika ushauri wa masoko kwa wamiliki biashara ndogo na kati hata
kubwa jinsi ya kuteka na kuwavuta wateja na kuongeza mauzo ya bidhaa kwa ada
Fulani ,kutokana huduma husika.
vii.
Mtafasiri wa maandiko mbalimbali kwenda
lugha ya wazawa;Kampuni nyingi za nje zinazokuja hapa nchini,huwa
wanahitaji kutafsiri taarifa zao kwenda lugha ya wazawa,mfano mradi
Fulani,tovuti zao,mfano kama ni kampuni ya vitabu mwandishi mmiliki angependa
ili auze kwa wazawa inabidi atafasiri kwenda lugha ya wazawa,Pia mfano kuna
hata miradi mbalimbali ambayo inatakiwaiangaliwe na wazawa nk.
viii.
Kutafiti fursa mpya za biashara,Nina
marafiki wangu ambao walianza kutoa huduma ya kutafi fursa mpya na wanafanya
vema kwenye hii biashara.Wanachofanya kutupia jicho kwa mambo
yajayo,mwelekeo,mahitaji aua fursa za biashara;na kuandaa mradi/mpango
kuhusiana hilo na kuuza hilo wazo kwa makampuni makubwa.Wakati mwingine
wanakuja na mawazo ya bidhaa na mawazo ya biashara yenye soko moja kwa moja
kubwa la kutosha;na kuuza hayo mawazo kwa makampuni kwa ajili ya
kuayaendeleza.Kama kazi hii unaipenda unaweza anza kutoa hudumu kutafiti fursa
mpya za biashara
ix.
Kutoa huduma za ku-print,Biashara
hii inafahamika sana na wengilakini bado inalipa sana.Unaweza kuanza kutoa
huduma ya ku-print business,banner sposters card,viperushi,flyers,catalogues
kwa biashara ndogo na za kati.
x.
Kutoa huduma za kuajiri,Siku
hizi kazi za managementi za rasilimali
watu kwa kampuni nyingi hutolewa na tenda kwa kampuni za nje ya kampuni husika
kufanya hiyo kazi ili kuongeza ufanisi kwa kampuni husika na hivyo kupelekea
kampuni husika kuweka umakini wake wa kutimiza lengo lake mahususi.Kama una
uelewa na ujuzi wa kutosha wa kushughulika na
maswala ya rasiliamali watu uwanja ni wako,kwa sasa hapa Tanzania
kujisajili kuwa wakala wa kuajiri ni bure unatakiwa uende pale wizara ya ajira
na vijana kujisajili.
xi.
Mshauri wa mitandao ya kijamii (social
media consultancy),Kwa hii dunia mitandao ya kijamii imechukua asilimia
kubwa sana.Je wewe unajua jinsi ya kutengeneza foleni kwa mitandao ya
kijamii?Unajua jinsi ya kuboresha na kuelimisha umma juu ya chapa(brand) za
makampuni ndani ya mitandao ya kijamii
kama facebook,twitter na linkedin?Basi unaweza kuwa mashauri wa mitandao ya
kijamii na kutengeneza fedha zako.
xii.
Kutoa huduma za kuandikisha majina ya
kampuni,Je wewe ni mzuri katika kuandika katiba za kampuni?unajua jinsi ya
kuchagua jina sahihi la kampuni?unajua
stepu zinazohitajika ili ukamilishe uandikishe jina la biashara?Anza sasa
fungua biashara yako ya kutoa huduma za kuandikisha majina ya kampuni .
Huduma
nyingine unaweza fanya ili kutengeneza fedha:
xiii.
Kutoa huduma za kuandikisha hakimili za bidhaa au huduma yako
xiv.
Huduma za ushauri kwa biashara ndogo
xv.
Kuandika kitabu kizuri na kukiuza kwa
umma.
0 comments: