Sidhani kama kuna asiyependa kuwa milionea.wengi wetu tumekuwa na
ndoto ya kufanikisha malengo yetu.Kuna
kitu kimoja cha kujiuliza hapo! Tunawezaje kufika hapo? Majibu yake ni mepesi
kuliko unavyoweza kuichosha akili yako kwa mawazo.Hizi ni baadhi ya njia tano
kuu za kukufikisha kwenye uwanja wa mamilionea!!!
Hizi ni baadhi ya njia tano kuu za
kukufikisha kwenye uwanja wa mamilionea!!!
1.Oa mara moja tu.
Njia hii inamwezesha mtu kuwa milionea
kwa kuwa na familia ya watoto wasiozidi watatu,na mke mwenye kuipangilia
familia bajeti ya kawaida!
2.Usiishi kwa kutegemea
kipato kimoja tu.
Kuoa ama kuolewa, ni kuunganisha pia nguvu kazi kati ya wawili hao. Hata
kama mmoja ana kazi na mwingine hana, mnaweza kuunganisha maarifa ya nini cha
kufanya ili kuwe na mfumo mwingine wa kipato cha ziada.
3.Chagua kazi au
biashara sahihi.
Iwe umeajiriwa au umejiajiri, hakikisha unachokifanya kinakulipa na
kutimiza baadi ya ndoto zako, ama zote ikiwezekana, (japo malengo huwa hayaishi.ukimaliza
hili,utawaza jingine).
4.Wekeza fedha zako
katika samani.
Tunashauriwa kuwekeza katika vitu vyenye thamani kuliko kuzitumia pesa
bila mpangilio.Maisha yanabadilika, na huwezi jua ni lini mkondo wako utayumba
na kuhitaji njia mbadala ya kukurejesha katika hali ya nyuma uliyokuwa nayo.Kwa
kununua mali zenye thamani, itakusaidia kwa kuviuza pale mambo yanapokwama, na
kuzitumia kuzalisha vingine na vingine zaidi.
5.Usiishi maisha ya
kimilionea.
Unaweza kuishi maisha ya kawaida na kwa muonekano wa kawaida katika macho
ya watu,kutakakokusaidia ku-maintain kipato chako vizuri kimatumizi.Kama
tunavyojua,ukiishi maisha ya juu,ndivyo mahitaji nayo yanakuwa ya hali ya juu.
0 comments: