Kwapa
ni moja ya maeneo yanayoweza kuleta karaha kutokana na baadhi ya watu kukabiliwa
na harufu inayofahamika kama ‘kikwapa’.
Zipo
sababu mbalimbali zinazochochea tatizo hili, moja kubwa kati ya hizo ni uvivu
wa kuoga na kuacha nywele nyingi kwapani. Wakati mwingine huachwa hivyo hadi
kubadilika rangi na kuwa nyeupe au njano na kujisokota.
Mtu
anapotoa jasho, bakteria wanatumia nafasi hiyo kwenda kwenye jasho
kujipatia chakula. Kadiri vijidudu hivyo vinavyozidi kuwa vingi harufu
nayo inazidi.
Kwa
kawaida, jasho lina kawaida ya kukaa kwapani zaidi kuliko sehemu yoyote mwilini
na kuwepo kwake eneo hilo kwa muda mrefu, husabisha harufu kali inayoweza
kusababisha mtu kukosa raha.
Baadhi
ya watu wamekuwa wakikabiliana na tatizo hilo kwa kutumia manukato na maji ya
marashi kuondoa tatizo hilo.
Hata
hivyo, kutumia manukato na maji ya marashi pekee, haviwezi kuwa njia pekee
yenye kuaminika katika kutafuta tiba na suluhu ya tatizo hilo
linalosababishwa na uchafu.
Moja ya njia za kukabiliana na
tatizo hilo ni kuoga maji mengi kwa kutumia sabuni iliyotengenezwa kwa kutumia
magadi. Kwa kiasi kikubwa, magadi yana uwezo wa kupambana na bakteria ambao
hujificha kwenye kwapa na kusababisha kutokea kwa harufu kali.
Pili ni muhimu kuhakikisha
kwapa linakuwa safi wakati wote, ikiwezekana kunyoa kila baada ya wiki moja na
baada ya kunyoa unaweza kupaka mafuta ya nazi ili kuondoa muwasho.
Njia nyingine ni unywaji wa maji mengi,
kwani kwa kiasi fulani yanasaidia kutoa sumu kwenye mwili na kusababisha harufu
kupungua.
Angalizo:
Kama unatumia kitaulo kujifuta maeneo ya kwapa hakikisha unakifua na kukianika kwenye
jua ili kuua vijidudu vinavyojificha kwenye nguo hiyo.
0 comments: