Takriban katika maisha
ya wanandoa walio wengi kama sio wote, ndoa zao hupitia katika vipindi tofauti.
Kama ulivyo umri wa Binadamu, ndoa hupitia katika kipindi cha utoto, ujana na
uzee, na kila kipindi kina mambo yake na taratibu zake ambazo kama wanandoa
watashindwa kuzifuata basi huenda ndoa hiyo ikakumbwa na mtihani mkubwa, nao ni
mtihani wa kuchokana.
Utoto wa Ndoa: Wengine
hukiita kipindi hiki (Honey Moon) mwezi wa asali, kipindi cha raha, utulivu,
mapenzi, maelewano baina ya wanandoa. Si lazima kiwe mwezi mmoja kama watu
wengi wanavyoamini, bali kinaweza kikawa chini ya mwezi mmoja au zaidi ya mwezi
mmoja.
Ujana wa
Ndoa: Hiki ni kipindi kinachofuatia baada tu ya utoto wa ndoa, ni
kipindi ambacho kila mmoja miongoni mwa wanandoa anakuwa tayari ameshamtambua
mwenzake katika shaksia yake (personality) kwa maana ya jinsi anavyoangalia
mambo, jinsi anavyofikiri, mitazamo yake, mielekeo yake na matarajio yake.
Uzee wa Ndoa:
Kipindi hiki ni kipindi ambacho wanandoa wanakuwa tayari wameishaingia katika
majukumu ya kulea kwa kupata matunda ya ndoa yao ambayo ni mtoto au watoto.
Kuchokana kwa wanandoa
ni tatizo ambalo linatokea kwa familia nyingi, na kusababisha migogoro mingi na
hata kufikia familia kuvunjika au kuishi kwa ajili tu ya kulea watoto na si
vinginevyo.
Utakuta katika baadhi
ya familia, Baba na Mama wanaishi katika nyumba moja, ukiwaona utadhani ni mume
na mke wanaopendana, kumbe wanaishi kwa ajili tu ya kuwalea watoto wao na
kuogopea maneno ya watu, hali hii ni hali ya talaka ya kimapenzi (emotional
Divorce) na ni hali mbaya ambayo mara nyingi humpa msukumo mwanamume wa kuoa
mke wa pili katika harakati za kutafuta utulivu na sehemu ya kukimbilia.
Tatizo hili la
kuchokana kwa wanandoa linasababishwa na wanandoa wote wawili kutokuwa na
uelewa wa kutosha juu ya haki za mume na mke.
0 comments: