HAWAHITAJI
mtu wa kuwachunga kwa ajili ya malisho au maji, hawana shida ya kumuona daktari
kwa ajili ya matibabu, hata mlinzi hawana haja naye, wenyewe ni hatari tupu kwa
adui yeyote atakeyesogea.
Gharama
ya kuwafuga haifikii ya ng’ombe, mbuzi, kondoo, au kuku. Wanyama hawa
wanahitaji fedha za kununua chakula, maji, na dawa ili kuhakikisha wanakuwa na
afya bora.
Mbali
na kutokuwa na gharama hizo, lakini nyuki wamekuwa wakimpatia Bahati Mhapa kitita cha zaidi ya Sh6
milioni kiulaini kila mwaka. Pia amekuwa akitumia asali kwa ajili ya matumizi
ya nyumbani.
Tofauti
na makundi ya ng’ombe, kondoo na mbuzi ambao kwa wale wafugaji wa kienyeji,
mchungaji hana budi kuambatana nao kwa umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta
malisho. Nyuki wamekuwa wakizunguka umbali wa zaidi ya kilometa 1,000 kwa ajili
ya kutafuta chavua wanayotumia kutengenezea asali.
Asali
inatajwa kama chakula kitamu zaidi kuliko mazao mengine yatokanayo na mifugo
kama nyama, maziwa, mayai n.k. Mbali na utamu kwa upande wa kula, lakini pia
asali inatumika kutibu magonjwa mbalimbali baada ya kuchanganywa na vitu
vingine.
Utamu
huo na matumizi hayo ndivyo vinavyompa nguvu Mhapa kujikita katika biashara hiyo huko kwao Mufindi mkoani Iringa
na kukusanya fedha za kutosha kutokana na mizinga 350 anayoitumia kuzalisha
asali. Lengo la Mhapa ni kufikisha mizinga 1,000 ifikapo mwaka 2013.
“Ninapata
wastani wa Sh1.5 milioni kila baada ya miezi mitatu na soko langu kubwa lipo
Dar es Salaam na Iringa, lakini hivi karibuni nimepata wateja kutoka Zambia
ambao wanaisifia sana asali hii,” anasema Mhapa wakati alipokuwa kwenye
maonyesho ya asali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Soko la asali
Mhapa anasema alipata zabuni kwenye shirika moja la Wajerumani ambao walikuwa wanataka lita 10,000, lakini bado hajaweza kufikia kiwango hicho, ndio sababu ana malengo ya kuongeza mizinga.
Mhapa anasema alipata zabuni kwenye shirika moja la Wajerumani ambao walikuwa wanataka lita 10,000, lakini bado hajaweza kufikia kiwango hicho, ndio sababu ana malengo ya kuongeza mizinga.
Wakati
Mhapa akinufaika, taarifa za Baraza la Asali Tanzania zinasema kiasi cha asali
kinachozalishwa bado ni kidogo licha ya mahitaji yake kuwa makubwa.
Katibu
wa Baraza hilo Dk Dansatan Kabialo, anasema jumla ya tani 9,380 zimekuwa
zikizalishwa kila mwaka, kiasi hicho ni sawa na asilimia saba tu ya uzalishaji
wa asali nchini.
“Kwa
kweli tunazalisha kidogo sana, ndio sababu tumeandaa maonyesho ili tukutane na
wadau mbalimbali wa asali na kuhamasisha wafugaji wafuge zaidi.
“Kwa
upande wa nta tunalizalisha tani 625.3 ambazo ziliingiza Sh2.8 bilioni kwa
mwaka wakati asali iliingiza Sh14 bilioni, bado ni kiwango kidogo tunataka watu
wajitokeze zaidi,” anasema Dk Kabialo.
Dk
Kabialo anasema soko la asali ya Tanzania lipo Falme za Kiarabu (UAE) Oman na
Iran, lakini kwa hapa Afrika asali hiyo ya kina Mhapa inauzwa zaidi Kenya,
Uganda na Rwanda.
Kwa
kuonyesha jinsi sekta hiyo inavyopiga vita umaskini nchini, Dk Kabialo anasema
kuwa sekta hiyo imeajiri watu milioni mbili nchini kote.
“Idadi
hii inahusisha warinaji, wauzaji, watengeneza vifungashio, watengeneza mizinga
na vifaa vingine vya ufugaji na urinaji wa asali,” anasema Dk Kabialo.
Asali
nyingi nchini inazalishwa katika mikoa ya Tabora, Dodoma, Kigoma na Singida.
Mikoa mingine iliyopo katika uzalishaji ni Iringa, Kilimanjaro, Arusha na Tanga.
Dk
Kabialo anatoa wito kwa wafugaji kufuata kanuni na taratibu za ufugaji nyuki
zilizowekwa na Serikali, lakini pia wajiunge na Baraza la Asali kwa ajili ya
kupata maelekezo zaidi.
Tiba
Kwa mujibu wa Dk Kabialo asali ina manufaa kwa watu wenye kikohozi, lakini pia ni nzuri kwa mtu aliyeungua na moto kwa kupaka kwenye majeraha yake.
Kwa mujibu wa Dk Kabialo asali ina manufaa kwa watu wenye kikohozi, lakini pia ni nzuri kwa mtu aliyeungua na moto kwa kupaka kwenye majeraha yake.
Mhapa
anasema mchanganyiko wa asali na mdalasini, unatibu ukungu wa miguu (fungus)
kwa kupaka sehemu iliyoathirika.
Dk
Kabialo anasema asali haiharibiki na kwamba inapokaa muda mrefu inaendelea kuwa
bora zaidi, hii ina maana unaweza kukaa nayo kwa zaidi ya miaka 30 bila
kuharibika endapo itahifadhiwa sehemu nzuri.
“Ikikaa
kwa muda wote huo, inabadilika rangi tu na kuwa nyeusi, ndiyo kwa sababu
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) hawakulazimishi kuweka tarehe ya
mwisho ya matumizi ya asali,” anasema.
Aina za asali
Zipo aina mbili za asali ya nyuki wanaouma (wakubwa) na nyuki wadogo (wasiouma), lakini Dk Kabialo anasema asali ya nyuki wadogo ni nzuri zaidi kwa sababu wana uwezo wa kupata chavua katika maua mengi yakiwamo maua madogo ambayo nyuki wakubwa hawawezi kuingia.
Zipo aina mbili za asali ya nyuki wanaouma (wakubwa) na nyuki wadogo (wasiouma), lakini Dk Kabialo anasema asali ya nyuki wadogo ni nzuri zaidi kwa sababu wana uwezo wa kupata chavua katika maua mengi yakiwamo maua madogo ambayo nyuki wakubwa hawawezi kuingia.
Dk
Kabialo na Mhapa wanasema mnyama aitwaye Nyigere ni adui mkubwa kwa sababu ana
uwezo wa kuangusha mizinga ili apate masega ya nyuki, sisimizi na mchwa nao
wakati wingine wamekuwa wakisababisha usumbufu ambao wanakula na kushambulia
mizinga.
Jinsi
ya kufuga nyuki
Nyuki wanatakiwa kufugwa eneo ambalo liko umbali wa mita 300 kutoka maeneo ambako kunafanyika shughuli za binadamu kwa sababu wakiwa karibu na makazi ya watu watawashambulia watu.
Nyuki wanatakiwa kufugwa eneo ambalo liko umbali wa mita 300 kutoka maeneo ambako kunafanyika shughuli za binadamu kwa sababu wakiwa karibu na makazi ya watu watawashambulia watu.
Nyuki
hawapendi harufu zenye manukato makali, hivyo kwa mtu ambaye amejipulizia
manukatao, anashairiwa asipipte karibu na mizinga ya nyuki.
Mhapa
amewataka wanawake wajitokeze kwa wingi shughuli ya kuzalisha asali kwani haina
gharama kubwa.
Lakini kwa upande wa Dk Kabialo anasema maonyesho ya nyuki yaliyofanyika jijini Dar es Salaam yamelenga kuwakutanisha wadau wa sekta hiyo wakiwamo watafiti ambao watatoka na azimio kwa ajili ya kuinua shughuli za ufugaji nchini.
Uchumi
wa Taifa na wa mtu mmoja mmoja unaweza kupanda haraka kwa kutegemea wadudu hawa
endapo malengo yatatimizwa.
Mmoja
wa washiriki wa maonyesho hayo ya asali Braitoni Kimaka kutoka mkoani Kigoma
anasema maonyesho yasifanyike Dar es Salaam tu bali yafanyike pia mikoani
ambako wapo wafugaji wengi.
Biashara hiyo inawezekana, nyuki ni wadudu wanaoweza kukupa utajiri.
Mimi Nina asali mbichi natafuta soko
ReplyDeleteUnapatikana wapi
DeleteNina asali mbichi zaidi ya litre 1000. Ni asali ya nyuki wakubwa 0762156929 namba yangu
ReplyDeleteNina asali mbichi zaidi ya litre 1000. Ni asali ya nyuki wakubwa 0762156929 namba yangu
ReplyDeleteNina asali natafuta soko 0714908121
ReplyDeleteNINA ASALI MBICHI NATAFUTA SOKO NAMBA YANGU NI 0768877559
ReplyDeleteNatafuta asali namba angu 0653371324
ReplyDeleteNatafuta hilo soko la asali huko falme za Dubai nipeni utaratibu wake jinsi ya kulipata hilo soko +255739367859
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteMimi huwa nanunua asali mbichi kwa ajili ya kusambaza, unaweza nicheki ukiwa na bei zako za jumla kwa ndoo za lita 20. Kama bei yako ni nzuri, basi tutafanya biashara, awamu ya kwanza ntachukua ndoo chache baadae uaminifu ukiwepo. Ntachukuza kati ya ndoo 50 hadi 100 au zaidi
ReplyDeleteAllen 0717188666 pia ipo WhatsApp
Mr habari? Nina asali mbichi nyuki wakubwa.0755369275.
Deletekaribuni nitaanza biashara ya asali wenye asali 0762268176 ila iwe nzuri pia iwe nje ya tabora
ReplyDeleteunaitaji asali kutoka wap wew
DeleteNapatikana tabora ni muuzaji wa asali 0756702701...karibuni sana
ReplyDeleteMam no vp?
DeleteNaomba kujua masoko ya asali kea hapa Tanzania
Kwa yyote alie serious na biashara ya asali anitafte 0762520328
ReplyDeleteKwa yyote alie serious na biashara ya asali anitafte 0762520328
ReplyDeleteMm mfuga nyuki asali kwagu muda wot kwa mawsiliano zaid 0620168841 rama mussa
ReplyDeleteMimi ni Kijana nataka kujifunza kuuza asali naweza nikapata msaada number yangu 0717165331
ReplyDeleteKwenye uzoefu wa asali inayotoka mbinga ruvuma tuonane ... Ina mchangsnyiko wa kahawa/coffee
ReplyDeleteinapendwa sana
Habari za sahizi, tuwasiliane number zangu 0758796889 au 0737769090 au 0717188666
Deletenahitaj kujua kuhusu asali siko lake,,upatkanaj wake..0767 068 818
ReplyDeleteHabr wapendwa nna asali ya kutosha natafta soko no 0655822814
ReplyDeleteHabar wapendwa nna asali ya kutosha natafta soko no 0655822814
ReplyDeleteNahitaji mtu wa kununua asali mbichi ipo ya kutosha
ReplyDeleteNahitji kunununua asali mwenye nayo anitafte 0712961234
ReplyDeleteHabari! Nina asali mbichi ni nzuri sana. Nitafute mteja. 0755369275.
ReplyDeleteNjoo vina food product morogoro kwa mahitaki ya asali
ReplyDeleteNdugu Unauzaje kwa liter moja ya asali iliyopikwa na mbichi.
DeleteNawaza kufanya biasha ya asali lakini sina elimu yakutosha kuhusu biashara hii,
ReplyDeleteNaweza kupata taarifa zozote kuhusu biashara hii?
Enter your comment...nauza asali mbich yenyewe ndio Lita 20= 190000 nicheck 0765146109
ReplyDeleteHello, Nina asali mbichi ya nyuki wakubwa pia nta ipo nyingi Sana nicheki 0653240453
ReplyDeleteHello habari Mimi pia ninafanya hii biashara ya Asali Mbichi ya nyuki wakubwa. Inatoka katavi nauza jumla Na rejareja nataman kujua masoko ya nje yapoje TUWEZE kuvusha kifupi namm natafuta soko maana asali ipo nyingi connection ndio shida
ReplyDeleteShukran Sana namba YANGU no 0653240453
Habari!!. Karibu tuweze kukupatia Asali ya Nyuki wakubwa kutoka Tabora,kwa Bei za Jumla na Rejareja 24/7. Phone 0625217177.
ReplyDeletewateja wako hasa wanatoka wapi? Je vipi kuhusu nta wateja wapo?
DeleteWanaoitaji Asali ya Nyuki wa Kubwa wanipigie hapa nauza kwa bei ya Jumla 24/7. Phone 0625217177.
ReplyDeletesoko la nta kwa hapa tanzania ni wapi ? na bei ya kilo moja ni shilingi ngapi?
ReplyDeletenaweza kujibiwa kupitia 0682023437
DeleteMimi Ni mfugaji naitaji kupata masponsa nnje ya nchi naomba mnipe njia pia
ReplyDeleteMimi ni mfugaji wa nyuki na muuzaji wa asali mbichi. Nipo bukoba mawasiliano 0766252546
ReplyDeleteHabari wajasiriamali wenzangu nina dumu 100 za asali lita 20 kama kuna anaehitaji nitafute 0768171124 nyuki wakubwa karibuni
ReplyDelete