Sauti siku
zote ina maana kubwa sana katika mtiririko wa wewe kujua mwenzako ana maanisha
nini. Sauti vilevile inaweza kukupa picha ya mzungumzaji jinsi alivyo
kutegemeana na ongea yake.Sauti huwezesha lugha yako unayoiwasilisha kueleweka
vizuri kwa msikilizaji endapo utaitumia ipasavyo.
Je wajua
sauti ya mtu kwa harakaharaka inamtambulishaje kwa msikilizaji?
• Mpole
• Mkali
• Hekima
na busara au
• Hasira
Linapokuja
suala la mahusiano,ni vizuri uzingatie matumizi ya sauti kutegemeana na muda na
hali Fulani ya maongezi.
Pale mnapokoseana,
ni vizuri ukatumia sauti yako kumshusha mwingine ili muweze kufikia
muafaka.Ukiendeleza sauti ya ukali hatakama haumaanishi kubishana, si rahisi
kufikia muafaka sanasana mtaishilia kuchukizana zaidi.
Sauti
hutumika katika kubembeleza ,yale mahadhi yakupanda na kushuka kwa sauti yako
humjengea mtu hisia na ladha Fulani tofauti na unapokua katika maongezi ya
kawaida au ya wewe na rafiki yako.
Unapokua na
mpenzio hakikisha unatumia sauti yako ipasavyo katika kunakshi maongezi yenu na
kuyafanya yawape furaha nakuwa na hamasa zaidi ya muendelezo wa mazungumzo au
shughuli nyingine bila kuchoka.
Siimaanishi
uige sauti ya Fulani,hapana.Bali kuwa mbunifu wa utumiaji wa sauti yako.
Kuwa
miongoni ya wale ambao wanapendwa kusikilizwa na wapenzi wao,sio kwa ajili ya
mapenzi ya dhati tu ,bali kwa jinsi wanavyoteka nafsi ya mwenziwe kwa matumizi
mazuri ya sauti yanayoipamba lugha na maongezi kwa ujumla.
Nadhani
ulishawahi sikia mtu anasifiwa kwa jinsi anavyoongea au umewahi kumsikia wewe
binafsi na akakufanya uvutiwe na ile hali.Jua unavyopangilia sauti yako
ipasavyo kutokana na mazingira na aina ya mazungumzo unapokua na mpenzi wako;
unamvutia (draw attention) na ni rahisi kwa yeye kukusikiliza and act
accordingly.
0 comments: