Images
Je..!! Unajua Tofauti ya Mjasiriamali na Mfanya Bishara Ndogo Ndogo... Soma hapa kujua tofauti zao
Watu
wengi wamekuwa wakitumia neno Mjasiriamali kama mfanya biashara ndogondogo,
kuna uhusiano baina ya ufanyaji biashara ndogo ndogo na Ujasiriamali, lakini
hakuna usawa kati ya vitu hivi viwili kwa dhana zifuatazo:
Kiasi cha Fedha na Utajiri.
Mfanya biashara ndogo ndogo mara nyingi hulenga kujipatia kipato cha kujikimu kutokana
na ukosefu wa kazi ya kuajiriwa au ugumu wa maisha na maisha huwa hayana
matarajio makubwa sana.
Mjasiriamali hufanya biashara au shughuli yake kwa malengo na matarajio ya
kujipatia kipato cha kutosha kujikimu, kufanya mambo ya maendeleo na hatimaye
kuwa tajiri Mkubwa kwa kuwekea mkazo shughuli zake kwa misingi muhimu ya
maendeleo.
Malengo na muda wa Mafanikio
Mfanya biashara ndogondogo anaweza maliza muda mrefu, hata maisha yake yote
ikibidi kwa kujipatia kipato kidogo sana, wakati Mjasiriamali huwa na ari na
kasi ya ya shughuli yake kwa kuwa na malengo na kuyaendea kwa kasi hiyo ili
kupata mafanikio na kujitengenezea utajiri ndani ya muda Fulani mfano ndani ya
miaka 3.
Hatari za kibiashara na kuziendea mbio nafasi.
Mjasiriamali huangalia hatari zinazoikabili biashara au shughuli yake na kuwa
na tahadhari za kutosha kujiepusha na madhara yanayoweza kuepukika ili azidi
kusonga mbele, pia huzitolea macho fursa zinazopita mbele yake au kwa wengine
na ku improvise(kuzinadia kwa upande wake) kwa mfanya biashara ndogo ndogo wa
kawaida hili halimshughulishi sana ili mradi anauza kidogo, na chakula
kinapatikana basi siku zinaenda.
Uvumbuzi na Ubunifu.
Mjasiriamali hufanya Uvumbuzi na Ubunifu zaida ya mfanya biashara ndogondogo wa
kawaida, uvumbuzi huu humpa changamoto zenye faida ambazo hupelekea kutajirika,
Uvumbuzi huu huwa katika bidhaa au huduma husika au katika utaratibu wa
kibiashara katika kufikisha kwa wateja/watumiaji wake.
0 comments: