Kuna hatua chache tu za kufuata kama unataka kuuza chochote kile; kwanza ni kumuonyesha na pengine kumfafanulia anayetarajiwa kuwa mteja wako kwamba kuna tatizo au kuna kitu kinakosekana, jambo la pili ni kumuelezea suluhisho la tatizo lake na jambo lingine ni kumfanya aamini kwamba wewe na bidhaa yako ndio suluhisho pekee au bora kwa tatizo/matatizo yake na mwisho ni kutoa suluhisho kwa makubaliano fulani.
kwa mfano kama wewe ni muuzaji wa vipodozi, unachotakiwa kufanya ni kumuelezea mteja wako mtarajiwa kwamba ngozi yake ingeweza kuwa bora zaidi[usije ukasema ana ngozi mbaya-utakosa kila kitu hata kama ni kweli],ingependeza na kuvutia zaidi na haswa anapovaa nguo zake nadhifu awapo ofisini au kwenye sherehe mbalimbali,baada ya hapo utaeleza jinsi wewe kwa utaalamu wako na kutumia bidhaa zako unaweza kufanya hilo likatokea iwapo tu mtakubaliana[kwa kuandika mkataba wa mauziano au kwa kupata oda toka kwake].
Jambo moja la kufahamu ni kwamba si lazima mara zote kupitia hatua hizi;kwa mfano mtu anapokwenda kununua kitu dukani kwa mangi[labda sabuni au mafuta ya kupikia] huna haja ya kufwata mlolongo huu,kwa sababu tayari mteja anajua tatizo na anajua suluhisho,kinacho bakia hapa ni makubaliano[bei] na kuuza.
jambo la pili,katika kuuza haswa bidhaa ngeni sokoni au yenye ugumu wa matumizi[complex] lazima utarajie vipingamizi[objections] kutoka kwa wateja watarajiwa. Kazi yako kama muuzaji ni kutoa majibu kwa vipingamizi muhimu tu atakavyo kuwa navyo mteja na kuchochea mhemko[hisia] za kufanya maamuzi haraka na si kujaribu kumshawishi mteja kwa maelezo marefu hata yale yasiyohitajika.
Kishawishi kikubwa wanachopata wauzaji[Sales Men & Ladies] ni pale wanapolowea[fall in love] kwenye kuelezea uzuri wa bidhaa zao na kusahau kabisa nini muhimu kwa mteja, na kwa kufanya hivyo mara nyingi wanaishia kushindwa kuuza kabisa.
Kazi muhimu ya muuzaji ni kugusa na kukidhi hisia za mteja baasi.Kwa lugha nyingine,ni kwamba pindi utakapoona umegusa hisia za mteja[kama ni mtaalam utajua tu wakati muafaka] huo ndio wakati wa kufanya makubaliano[close the sale],si wakati wa kuendelea na hadithi kuhusu bidhaa yako.
0 comments: