Fursa ni mapengo ya
mahitaji yaliyoko katika jamii yanayohitaji kuzibwa. Kwa maana ingine fursa ni hitaji, nafasi au
changamoto au mazingira fulani ambayo mjasiriamali hutumia kuibua wazo la
biashara. Wazo la biashara ndio chimbuko la biashara.
Mjasiriamali ana mazingira
yanayomsaidia kutambua fursa ya biashara.
a) Mazingira
ya ndani/Maisha binafsi
-
Mjasiriamali anapaswa kuangilia maisha yake binafsi.
- Kazi
alizowahi kufanya huko nyuma
- Mambo
unayoyapenda kufanya mara kwa mara
b)
Mazingira ya nje
-
Watu wanaokuzunguka
-
Maeneo unayopenda kutembelea mara kwa mara
-
Mahitaji ya jamii unayoyaona
Njia zifuatazo humsaidia
mtu kutambua fursa ya biashara
1.
Vyombo vya habari kama magazeti, redio, TV.
2.
Mitandao ya Komputa yaani Inteneti
3.
Majarida
4.
Maonesho ya biashara
5.
Machapisho ya magari
6.
Mazungumzo
7.
Kusafiri sehemu moja hadi ingine
8.
Mihadhara
9.
Kufuatilia sera ya nchi mfano kilimo kwanza
10. Kutembelea taasisi za
biashara
11. Watoa ushauri kuhusu
biashara
0 comments: