Images
Utafanyaje Ukivutiwa na Mpenzi Mwingine
Wapo watu ambao wameoa au
wana wapenzi walioahidiana kwa mambo mengi, lakini wamekuwa wakikabiliwa na
tatizo la kuvutwa kimahaba na watu wengine. Hali hii huwatokea wawapo masomoni,
kazini, kwenye biashara,mbali au pengine
hata karibu na wenza wao wa zamani.
Sayansi ya jamii inakubali kuwa mwingiliano wa
kijamii mara nyingine huathiri tabia za watu,ukweli huu unathibitishwa na
ongezeko la usaliti katika mapenzi, mantiki
ikibaki kwenye mwili kulazimishwa na mapokeo ya tafsiri ya vitu vinayotawala
mawazo ya mwanadamu.
Maelfu ya wanaume na wanawake hulazimika kuwasaliti
wapenzi wao baada ya kuvutiwa na maumbo au sura za wanaume/wanawake wanaokutana
nao katika shughuli zao za kimaisha.
Wapenzi hao hujikwaa kupitia macho na hisia
zao,huku wengi wakikiri kushindwa kuzuia matamanio
“Msichana/mvulana huyu ni mzuri sana nahisi
kumpenda, nimuonapo nachanganyiwa kabisa.”
Inawezekana hata wewe unayesoma makala haya umewahi
kutamka maneno haya na ukasahau kuwa umeoa/ umeolewa au una mchumba uliyepanga
kufunga naye ndoa.
Kama hilo halitoshi yawezekana umeshakuza mawazo
hayo kiasi cha kuona huna jinsi zaidi ya kufanya usaliti, ukatongoza au ukajitongozesha kwa gharama ili
utii hisia zako.
Ninapotazama mwenendo wa wapenzi wengi siku hizi,
nabaini kuwa mihemko ya miili inawaangusha wengi kwenye usaliti, jambo
linalonifanya nilazimike kufundisha namna ya
kukabiliana na tatizo hili ili kuweza kuyanusuru mapenzi.
Naliita jambo hili tatizo kwa sababu limeleta
madhara mengi katika jamii, kuna watu wameshauana, ndoa kusambaratika na mapenzi kufa, isitoshe uchunguzi
unaonyesha kwamba, wasaliti wengi hawakupata faida au raha waliyoitarajia
kutoka kwa wale waliowashawashi, hivyo
kufanya hisia zao ziwe kazi bure.
Naamini hakuna mwenye akili timamu anayependa
kupoteza utu wake bila faida. Ndiyo maana ipo orodha ndefu ya watu walionifuata na kukiri: “Alinirubuni
nikamwacha mpenzi wangu, kumbe alitaka kunichezea tu.” Wanakiri kurubuniwa, lakini wanasahau kuwa walikubali
baada ya kuvutwa na hisia! Je mpaka sasa ni
wanaume wangapi wanavutwa kimahaba na akidada warembo wanaokutana nao kiasi cha
kuwapuuza wapenzi wao wa zamani na kuamua
kuwasaliti?
0 comments: