Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Familia bora hutegemea Muongozo mwema wa Wazazi Kwani wao ndiyo Walimu wa kwanza kwa Mtoto




Kama inavyojulikana wazazi wawili ndiyo muongozo wa familia, baba akiwa kichwa cha familia akifuatiwa na mama. Siku zote familia bora hutegemea muongozo mwema wa wazazi, kwani wao ndiyo walimu wa kwanza kwa mtoto.

Siku zote watoto hujifunza kupitia wazazi wao wanachokifanya ili nao wakitumie kama dira ya maisha yao pindi wakifikia umri wa kujenga familia zao. Kama muongozo utakaowafanya waweze kuishi muda mrefu katika maisha ya ndoa na kifo pekee ndicho kitakacho watenganisha.

Katika maisha ya kila siku ya mwanadamu hawawezi kuishi kama malaika, ipo siku wanaweza kukosana kwani makosa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Ndiyo maana tumefundishwa kusamehe au kuomba msamaha pale unapojua umekosa.

Lakini kuna baadhi ya familia zimekuwa zikiwashirikisha watoto wao katika matatizo yao pindi wakosanapo, ikiwamo kufokeana mbele yao pindi wazazi wanapo tibuana.


Mnashindwa kutafuta sehemu ya faragha na kuonyana kiutu uzima, kama wazazi ambao siku zote watoto hutakiwa kujifunza mazuri kutoka kwenu. Kufokeana mbele ya watoto mnawafundisha nini?

Inapotokea baba au mama anapokuwa akimtumia mtoto wake kujua kama mwenzake kuna kitu kibaya amefanya kwa kumuuliza: “Ulipotembea na baba yako hakuzungumza na wanawake?” Au baba kukuuliza “Nilipokwenda kazini mama yako alitoka au alizungumza na mwanamume?”

Nina imani kwa mawazo yenu unajiona mpo sawa kumbe sivyo, kwa mtindo huu inaonyesha ndani ya uhusiano wenu hakuna uaminifu. Hamuwezi kumfanya mtoto kama mlinzi wa mmoja wenu. Hivi mnamfundisha nini au ndiyo mnajionyesha jinsi gani msivyo aminiana.


Kwani mtoto huamini matatizo ndani ya familia ni msiba mzito ambao mwisho wake ni wazazi kutengana na kuweka mpasuko katika maisha yake. Mzazi mwenye busara siku zote hukanyana sehemu ya faragha ambayo humfanya mtoto aamini siku zote wazazi wake hawana matatizo.

Pia kama una wasiwasi na mwenendo wa mwenzako kwa nini usimwite mkae chini na kutatua kwa busara, kwani hakuna mwanadamu aliyekamilika asilimia mia.

Familia bora ni ile ambaye inahakikisha matatizo yao hayaathiri watoto wao, hutatua kwa busara huku wakizingatia watoto wao wanawategemea wao. Wazazi kuweni walimu wema katika familia zenu ili kujenga familia yenye maadili mema.



0 comments: