Kabla sijatoa sample, ni vyema
tukatambua kuwa bajeti ina makundi matatu ya muhimu: Mambo ya lazima ambayo
huwezi kuahirisha,Mambo ya ziada ambayo unaweza kuahirisha na Mambo ya dharura
usiyoyatazamia.
Mambo ya Muhimu
Haya ni matumizi ya lazima kila siku
ambayo unaishi, ni ya lazima ili wewe na familia yako muendelee na maisha. Hapa
ndipo unapopaswa kuweka hela yako kabla ya mambo yote mengine.
- Fungu la kumi na matoleo yote.
- Bili zote (kodi ya nyumba, umeme, maji, insurance, ada, wasaidizi wa kazi,ulinzi).
- Chakula (nyumbani, kazini).
- Usafiri (mafuta ya gari, nauli).
- Matumizi muhimu ya nyumbani (sabuni, mafuta, pampers kwa wenye watoto, vifaa vya usafi).
Mambo ya Ziada
- Nguo na Viatu
- Kulipia vitu vya ziada kama Dstv, gym, na membership nyingine
- Kutoka na familia kwenda kupumzika mahali
- Michango ya harusi ma sherehe
- Michezo ya watoto na zawadi nyinginezo
- Saluni
Matumizi ya Dharura.
- Hospitali
- Michango ya majanga
Ukishaainisha matumizi yako kwenye
makundi haya, ndio utajua lipi la ziada ufanye na lipi lisubiri wakati
mwingine, na ukiweka hela ya akiba kwa ajili ya dharura. Utashangaa kwa nini
nimeweka kodi ya nyumba na ada kama matumizi ya mwezi wakati unalipa mara moja
au mbili kwa mwaka. Wengi tunakosea hapo, unatumia hela yote kisha ukifika
wakati wa kulipa kodi unatafuta pa kukopa. Kodi yako unatakiwa kuilipa kila
mwezi ila tu mwenyenyumba anaitaka kwa mkupuo, ili usiangaike baadaye hakikisha
kila mwezi unaitoa pamoja na ada zote na kuweka pembeni hasa kwenye akaunti
maalumu. Ukifika wakati wa kulipa unakuwa huna wasiwasi.
Usije ukanunua nguo, viatu au kuitoa
familia out wakati haujatoa fungu la kumi, hujalipia umeme au hujatenga kodi ya
mwezi husika. Wengine wanashona kitenge kila kitchen party na kwenda saluni
kila wiki na nyumbani hajui wiki ijayo atakula nini. Fanya shopping ya mwezi,
ya kila kitu ambacho hakiharibiki: sukari, unga, mchele, majani ya chai,
sabuni, dawa za miswaki, tambi, maharage, mafuta, pampers, wipes, maziwa n.k.
Utakuwa na maisha ya furaha sana, na vitu kama nyanya, nyama, vitunguu, karoti
unanunua kwa wiki. Yani kwangu kitu ninachonunua kwa siku ni mboga za majani na
ndizi tu.
0 comments: