Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Je..!!! Unataka kuanzisha Biashara ya Mkaa... Soma hapa upate Muongozo mzuri katika Biashara yako hiyo ya Kuuza Mkaa.




Ni muda muafaka sasa kwa vijana waliomaliza masomo kutafakari kujiajiri badala ya kuajiliwa. Leo hii nitazungumzia jinsi ya kuanzisha biashara ya kuuza mkaa. Mambo nitakayoangalia  ni kama ifuatavyo:

  • Mahali pa kufanyia biashara
Nitahakikisha kuwa ninapata sehemu nzuri ya kufanya biashara (sio uchocholoni) ambapo kuna nafasi ya kutosha kufanya biashara na pana usalama wa kutosha kwa bidhaa, vitendea kazi na pesa pia
  • Eneo la kufanyia biashara pana wateja wengi
Nitahakikisha eneo nitakalochagua kwa biashara (sio Masaki au Oysterbay) lina wateja wa kutosha kunua mkaa wangu. Ninafahamu kuwa bila ya wateja hakuna biashara, kwa hiyo nitakuwa makini kwa suala hilo

·         Upatikanaji mkaa

Itabidi nihakikishe kuwa ninapata mkaa wakati wowote, isije ikatokea wateja wangu wanahitaji mkaa wakati ampapo duka langu halina mkaa
  • Upatikanaji wa Mkaa mzuri
Nitahakikisha kuwa mkaa wangu utakuwa mzuri (sio wa mikorosho) kwa maana unawaka vizuri na unadumu kwa muda mrefu. Nisingependa wateja waache kuja kwangu kwa kuwa nauza mkaa mbovu ambao unaungua na kuisha haraka kabla ya kuivisha chakula
  • Bei ya kununua na kuuza mkaa
Nitahakikisha nanunua mkaa kwa bei nafuu ili niweze kuuza kwa wateja kwa bei nafuu na wakati huo huo nipate faida
  • Mtaji wa biashara
-  Nitahakikisha nina mtaji wa kutosha utakao wezesha kufanya yafuatayo:
-      Kulipia pango la sehemu ya biashara
-      Kununua mkaa wa kwanza kuanzisha biashara
-      Kununua vitendea kazi kama ndoo, beleshi, nguo, apron na kadhalika
-      Akiba kwa ajiri ya dharura
  • Uwekaji wa hesabu za biashara
Nitakuwa na utaratibu wa kuweka kumbukumbu za manunuzi ya vitu, malipo mbali mbali, pesa za mauzo na kadhalika. Kumbukumbu hizo ndizo zitakazosaidia kutengeneaza hesabu zitakazoonyesha kama biashara inaendeshwa kwa faida au hasara
  • Weka pesa zako benki
Hakikisha pesa baadhi  zinazotokana na biashara ya mkaa zinawekwa benki kwa mahitaji yako ya baadae.

Biashara njema…


4 comments:

  1. aisee bro pole sana. unawezaje kuandika article nzima based on your merely on yo day dreaming (wishful thinking)in the name of giving people exposure.There is no fraction of experience, skills, strategy or watsover. all is abt wat you opt you should do lol...such a thing normally remains in the brain bro..ts a shame talking abt it thinking you are empowering people with t.its the first thing i have found on the internet since 9/11. regards.

    ReplyDelete
  2. Mkaa unaweza kutoa makopo mangapi gunia moja

    ReplyDelete
  3. Natakiwa nianze n mtaji wa beigan au gunia ngap?

    ReplyDelete
  4. Kunauhitaji wa kufanya mazungumzo na maliasili

    ReplyDelete