“Kusema ni rahisi
kuliko kutenda!” Ndivyo watu wengi husema juu ya kujifunza lugha ya kigeni,
hasa baada ya kujaribu. Ni kweli kwamba, kujifunza lugha nyingine ni jambo gumu,
bila kutia chumvi. Lakini wale ambao wamefanikiwa wanasema kwamba jitihada hiyo
yastahili.
Utahitaji nini ili ufanikiwe kujifunza lugha ya kigeni?
Wengi ambao wamefanya hivyo wanakazia mambo yafuatayo.
● Kichocheo. Unahitaji kichocheo—sababu ya
kufuatia mradi wako. Wanafunzi wenye kichocheo kikubwa kwa kawaida hufanikiwa.
● Unyenyekevu.
Usitazamie kutimiza mengi mno—huwezi kuepuka makosa, hasa mara ya kwanza. Watu
watakucheka kwa hiyo hata wewe cheka. Unakuwa kama mtoto ajifunzaye kutembea.
Mara nyingi utajikwaa, lakini lazima tu uamke na ujaribu tena.
● Subira. Miezi ya mwanzo itakuwa migumu, na
nyakati nyingine uta taka hata kukata tamaa. Hakikisha unafanya maendeleo mpaka
unapokumbuka yaliyopita.
● Mazoezi.
Utaratibu wa kawaida utakusaidia kusema lugha mpya kwa ufasaha. Jaribu
kujizoeza kila siku, hata kama ni kwa dakika chache tu. Kama vile kitabu kimoja
kikuu kisemavyo, “‘mazoezi machache kwa ukawaida,’ ni afadhali kuliko ‘mengi
lakini mara mojamoja.
Je, uko tayari kukubali ugumu wa kujifunza lugha ya kigeni?
Ikiwa ndivyo, vifaa vifuatavyo vyaweza kuongeza ubora wa maendeleo yako.
● Kadi
za kujifunzia. Kila moja ya hizo ina neno au kifungu cha
maneno mbele na tafsiri yake nyuma. Ikiwa hazipatikani mahali unapoishi,
unaweza kufanyiza zako mwenyewe kwa kutumia katalogi ya kadi.
● Kaseti
na vidiokaseti za maagizo. Hizi zaweza kukusaidia usikie lugha
ikisemwa kwa usahihi. Huku ukijaribu kwa maneno yanayo kutatiza kuyatamka.
● Programu
za mawasiliano ya kompyuta. Baadhi ya hizo hukuruhusu urekodi sauti
yako na kulinganisha matamshi yako na wasemaji wenyeji wa lugha hiyo.
● Redio
na televisheni. Ikiwa kuna programu za redio au televisheni mahali
penu zinazotumia lugha unayojifunza, kwa nini usifungulie na uone ni kadiri
gani unaweza kujifunza?
● Magazeti
na vitabu. Jaribu kusoma habari iliyochapishwa katika lugha mpya,
ukihakikisha kwamba kiwango cha kuelewa si cha juu zaidi au cha chini zaidi.
Kuielewa Kabisa
Lugha Hiyo
Bila shaka, baada ya
muda mfupi au baadaye itakubidi uzungumze na wale wanaosema lugha hiyo.
Huhitaji kusafiri nchi ya mbali. Badala yake, labda unaweza kutembelea kutaniko
linalosema lugha ya kigeni.
0 comments: