Katika maisha kuna mambo mengi sana ambayo unayatamani, na kila siku unaomba yawe mikononi mwako. Tangu ulipoanza kuyatamani ulikuwa na mipango, mawazo na mikakati mingi sana kichwani, lakini mpaka leo haujafanikiwa kuwa nacho. Na yawezekana unajiuliza kila siku na jibu mpaka leo haujapata. Sasa hebu leo chukua hizi hatua nane halafu anza kuzifanyia kazi:
1.ANZA KUKAA NA WATU SAHIHI
Hawa ni watu ambao wewe unapokuwa
nao unafurahia, wanaokupenda, kukuthamini, na wanaokutia moyo wa
kutokata tamaa katika mambo yako.Hawa ni wale watu ambao ukikaa nao wanakufanya
ujihisi uko hai, ambao wanaokukumbatia wewe wa sasa hivi na wanaotamani
kumkumbatia yule unayetamani kuwa, bila masharti yoyote.
2.ANZA KUWA MUAMINIFU KWA NAFSI YAKO
Kuwa muaminifu kwa jambo lipi ni
sahihi kwako, na lipi linahitaji kubadilishwa. Kuwa muaminifu kwa lipi unataka kufanikisha
na nani unataka kuwa. Ukianza kujidanganya nafsi yako mwenyewe utakuwa
unakosa fursa za kujitambua kama unachotamani ni sahihi kwako.
3.ANZA KUTENGENEZA VIPAUMBELE VYA
FURAHA YAKO
Mahitaji yako yana umuhimu
sana. Kama usipoanza kuweka vipaumbele vya vitu gani hasa vinakupa furaha,
hautaweza kujitambua wewe ni nani. Kama utaweza kutambua wewe unafurahia
nini itakuwa rahisi kuwafurahisha na watu wako wa karibu.
4.ANZA KUWEKA WAZI WAZO NA NDOTO
ZAKO
Katika maisha, kama unasubiri fursa
zikufuate utangoja milele, lakini kama ukiziuata fursa huko ziliko
zitakupokea kwa mikono miwili. Haina maana kukaa chini na kujisifu kuwa
una mawazo na ndoto nzuri, kama haujaanza kuzitoa zionekane.
5.ANZA KUJIVUNIA ULIVYO
Kama haujaanza kujivunia vile ulivyo
leo, itakuwa ngumu kupiga hatua zako mwenyewe kuelekea mafanikio. Ukianza
kujivunia vile ulivyo utafanya uyaone mawazo yako yana thamani, nguvu na uzuri
ambao hakuna mwengine yeyote anao.
6.ANZA KUJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA
Kama uliwahi kukosea na ukapata
funzo fulani anza kulithamini hilo funzo kwa kuchukua mafundisho yake
na kuyafanyia kazi. Na ukiweza kufanya hilo, utaona kumbe kukosea ni hatua
moja wapo katika kupata mafanikio. Kwani kuna uwezekano mkubwa kabisa kama
usipotaka kujifunza kutokana na hilo basi utakuwa unalikwepa daraja
ambalo lingekuunganisha na mafanikio.
7.ANZA KUWA MKARIMU KWA NAFSI YAKO
Kama utaendelea kutumia muda mrefu
katika kuilaumu nafsi yako, na kutaka kujiadhibu utakuwa unaendelea kujirudisha
nyuma. Ukiwa mkarimu kwa nafsi yako utaona nafasi ya wewe kunyanyuka kila unapokuwa
umedondoka bila kujikatisha tamaa.
8.ANZA KUSHUGHULIKIA MATATIZO YAKO
Matatizo yanayokukabili hayatoi
tafsiri ya wewe ni nani, bali jinsi unavyoyakabili na kuyamaliza
ndiyo tafsiri yako ilipo. Matatizo hayawezi kuondoka mpaka wewe mwenyewe
uyakabili. Fanya jitihada zako zote pale unapoweza halafu jipongeze kwa hatua
uliyopiga.
0 comments: