Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Jihadhari na vituo visivyotoa habari kamili kuhusu kazi internet





Kutoa habari kuhusu elimu na ujuzi wako kwenye Intaneti kutafanya watu wengi zaidi wanaoweza kukuajiri wapate habari hiyo, lakini unahitaji kujihadhari. Pia kunaongeza uwezekano wa kulaghaiwa. Ili ujilinde na jambo hilo, wataalamu wa vituo hivyo wanashauri hivi:
1. Soma maagizo ya kuweka siri ya kituo kinachotangaza nafasi za kazi kabla ya kutoa habari kuhusu elimu na ujuzi wako. Vituo fulani vya kusaidia watu kupata kazi huuza habari zako za kibinafsi kwa kampuni nyingi au kwa watu wengine.
2. Toa habari kuhusu elimu na ujuzi wako kwenye vituo vichache tu vya Intaneti vyenye sifa nzuri vinavyosaidia watu kupata kazi. Unapaswa kulinda habari zako za kibinafsi ili zisitumiwe vibaya. Habari utakazotoa hazipaswi kutia ndani habari ambayo mwizi anaweza kutumia na hivyo kukuletea matatizo mengi ya kiuchumi. Waajiri wanyoofu hawahitaji kujua namba ya akaunti yako ya benki, namba ya kadi yako ya mkopo, au tarehe yako hususa ya kuzaliwa.

3. Jihadhari na vituo visivyotoa habari kamili kuhusu kazi. Pam Dixon, mtafiti anayefanya kazi na shirika la World Privacy Forum, anasema kwamba kituo kikitoa habari zisizo kamili, huenda kazi hiyo si halali. Anaongeza hivi: “Maneno yasiyo wazi kama ‘Tuna nafasi nyingi sana za kazi’ au ‘Sisi hushirikiana na kampuni kubwa’ yanapaswa kuwa onyo. Pia jihadhari ukiombwa utume tena habari kuhusu elimu na ujuzi wako.”
  Kumbuka, hata vituo vyenye sifa nzuri vinavyosaidia watu kupata kazi haviwezi kuamua jinsi habari zako zitakavyotumiwa baada ya kuchukuliwa na mtu anayeweza kukuajiri au watu wengine.




0 comments: