"Mimi ni mwanamke wa 25 nimeolewa miaka 3 iliyopita
kwa sasa ni mjamzito hivyo niliacha kwenda kazini tangu mimba hii ilipoingia
kutokana na matatito ya kiafya. Mume wangu ana nafasi nzuri kazini na kipato
chake kinakidhi mahitaji ya familia yetu.
Baada ya matumizi muhimu kwa kawaida najua anabakisha
kama laki 5 kila mwezi lakini hakuwahi kunijulisha kama ana pesa hizo au ana
plan gani na mabaki hayo ya pesa, nikimuuliza anasema hana pesa.
Wakati huo mimi kuwa baada ya mahitaji muhimu najua pesa
fulani hubaki na sasa amefikisha million 5 lakini hataki kusema ukweli, Pesa
hizo zipo kwenye account nami najua password yake lakini yeye hatambui hilo.
Je mtu wa aina hii nimchukulie kama alivyo au nimweleze
ukweli"
Jawabu: Asante kwa ushirikiano wako,
inaonyesha wewe ni mmoja kati ya wanawake wachache ambae ulikuwa ukijituma ili
kuchangia kipato ndani ya nyumba na ninachokiona hapa ni ile hali ya
"kujishitukia" kwa vile hufanyi kazi unafikiri mume wako
atakunyanyasa na bila kujijua unaamua kuomba pesa ambazo pengine wala
huzihitaji....kama ulivyosema mwenyewe kuwa anakamilisha mahitaji yote muhimu.
Kitu kingine ninachokionahapa ni kuwa na hofu kuwa
anaweza kuwa anazitumia pesa zinazobaki kwa ajili ya mambo mengine kama vile
"kuwekeza" kwenye Ulevi na wanawake nje ya ndoa yane kwa vile tu wewe
ni mjamzito (kutokana na matatizo ya kiafya ni wazi kuwa tendo la ndoa halipo
vile inavyotakiwa kitu ambacho kinaongeza hofu).
Lakini kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa pesa zote
zinazobaki baada ya mahitaji muhimu anazitunza Benk, hazitumii kivingine.
Kumbuka wewe ni mjamzito which means kuna "mtu" mwingine ataongezeka
kwenye familia yenu ndogo na badala ya kuwa wawili mtakuwa watatu nahivyo basi
majukumu yataongezeka na kwa mshahara wa mtu mmoja tu mtoto hatokuwa na maisha
bore.
Sasa ili mtoto kuwa na maisha bora au angalau
"comfortable" ni wazi kuwa kuna ulazima wa ninyi kama wazazi
kujiandaa na jukumu hilo jipya. Si hivyo tu bali kuna matukio ambayo hujitokeza
bila mipango kama sehemu ya maisha yetu yanaitwa "udhuru" ni wazi kwa
akiba inahitajika incase kitu kama hicho kinaibuka.
Sote tunapokuwa na mipango fulani na pesa tunazotunza
ili kukamilisha jambo fulani alafu mtu akaibuka na kukuomba seti au kukuazima
ni wazi kuwa utamwambia kuwa huna pesa....sio huna kabisaaa bali ulizonazo
zinamipango yake muhimu na hutaki kuzigusa unless upate "udhuru" kama
kuuguliwa, msiba n.k.
Umchukuliaje?-Since unalo neno/namba ya siri ya Benki
Akaunti basi mchukulie kuwa ni mmoja kati ya mwanaume wachache wanaojua
majukumu yao, anangalia mbele na sio pale mlipo (kuvaa miwani ya mbao) pia ni
muaminifu na ndio maana akakupa neno/namba ya siri ya account (natumai
hukuitafuta mwenyewe balia likupa baada ya kuomba).....vinginevyo mume wako
anajaribu kufanya mambo yake kama mwanaume na wewe unapaswa kumuamini.
Nini cha kufanya-Hakuna ukweli wa kumuambia hapo
kwasababu moja, Pesa ni zake, Pili hazitumii bali ziko pale zimetulia, tatu
wewe unataka pesa za nini wakati kila kitu unatimiziwa ndani ya nyumba?
Kama unawasiwasi sana na wewe ni mwanamke kamilifu na
mke hivi sasa ni lazima ulifunzwa namna ya kupata unachotaka kutoka kwa mume
wako kwa kutumia lugha ya kimapenzi (siwezi kusema hapa kwani kaka zangu
wakijua hatutopata kitu), sasa tumia mbinu hiyo kwa mume wako na hakika
atakueleza mipango yake kuhusu pesa hizo (akiba) na hapo utapata amani moyoni
mwako.
Acha kujishitukia kwa vile umeacha kazi, jiamini hali
itakayokusaidia kumuamini mume wako.
0 comments: