Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Kama una Dalili Hizi basi Utakuwa na Mapepo.. Je..!! Unataka kuzijua dalili hizo soma Hapa..



Kuhusu majini kuna majini wema na wabaya
(a) Majini wema.
1.Majini wema awamuingii mtu na kumlazimisha mambo kwani hiyo ni dhuluma.

2.Humpatia mtu mambo mazuri yale anayo hitaji mtu mwenyewe kwa mfano:- utajiri na Nk.

(b) Majini wabaya ni wale waliomuhasi mungu hao hujiita mashetani.
1.humuingia mtu au hukaa maeneo anayoishi
2.Hutumika na watu wabaya kuwapelekea watu wengine,kuaribu maisha ya mtu au asifanikiwe na jambo fulani.

Dalili unapokuwa macho(ukiwa hujalala)

1.Kujisikia unachukia kufanya Ibada
2Kufanya makosa makosa katika kauli(maneno) , kutembea kwa kuangukaanguka

3.Kuanguka kama kifafa bila ya kuwa na ugonjwa wa kuanguka kifafa nah ii ni moja katika dalili za kupatwa na jinni ima la kutupiwa au jinni la upepo mbaya(pepo mbaya)

4.Miguu kuwa haina nguvu(kupalalaizi) bila sababu maalum ya kitabibu

5 Kuwa na hasira bila sababu , au kulia bila sababu ya msingi

6.Kukaa chooni kwa muda mrefu na kuongea pekee yako na kujijibu

7Kuumwa kichwa mara kwa mara , na kichwa hakitulii hata ukinywa vidonge

8.Kwa upande wa wanawake kutokwa damu bila mpango maalum wa siku zao, angalizo katika hili kuna wanawake wenye Anemia wamuone daktari kwanza.

9.Kutokupata watoto, ingawa mume na mke wote ni wazima na wana uwezo wa kuzaa
Kuna dalili nyingi mno ila hizi ni katika hizo dalili

Dalili unapokuwa usingizini
1.Kupata ndoto za kutisha , ambazo zinakufanya kuona viumbe vya ajabu na vya kutisha, kujiona unaanguka toka ghorofani au unaanguka katika shimo, kuona nyoka usingizini.Kuota kuingiliana kimwili na mtu usiyemfahamu na kumuona mtu anakutisha usingizini

2.Kuwa msahaulifu , kuwa na wasiwasi, na kuwa muoga (unakuwa mwoga)wakati wa kuamka

3.Kuongea kwa sauti kubwa(kupayuka) ukiwa usingizini. Aya za kumsomea Mgonjwa aliyepatwa na jinni wa kutupiwa au jinni wa upepo mbaya(pepo) pia ayah hizi zinaandikwa kama Kombe kwenye karatasi safi na kulowekwa na kupewa mgonjwa kunywa na kujipaka mwilini kwa muda wa masiku ambayo tiba yake itakuwa ianendelea.Tiba hii ni kunywa , kujipaka na kusomewa.Aya hizi pia huweza kutumika kuweka kwenye mafuta ya Zaituni ili mgonjwa awe anajipaka







1 comment: