Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Wanaumia sana mioyo yao ama kukosa penzi la kweli au kuingia katika penzi la kitapeli wakiamini ni penzi la dhati... Soma hapa

Romantic Black Art Page 1

Wengi wamekuwa wakiumia sana mioyo yao ama kukosa penzi la kweli au kuingia katika penzi la kitapeli wakiamini ni penzi la dhati. Tatizo hili limekuwa likiwasumbua wengi, inawezekana hata wewe limewahi kukukuta au upo katika tatizo hili hivi sasa.


Tatizo hili husababishwa na kukosa umakini ikiwa ni pamoja na kutofuata taratibu sahihi kabla na baada ya kuanzisha uhusiano wa mapenzi. Hapa sasa ndiyo chanzo cha matatizo.

Unapokuwa na simanzi ni wazi kwamba kila kitu kitakuwa hakiendi sawa, maisha yanabadilika, kila unachokipanga kinavurugika, ufanisi wako kazini unashuka.

Siyo ajabu, bosi wako anafikiria kukufukuza kazi kutokana na kuboronga ofisini. Kimsingi simanzi ni tatizo sugu katika maisha ya kiuhusiano na ni vyema ikiwa umejifunza mapema jinsi ya kuepuka simanzi katika maisha yako ya kimapenzi.

Kuna mambo mengi ambayo wengi huyakwepa ama kwa kuyajua na wakati mwingine bila kujua kuwa wanakosea na mwisho wanajisababishia simanzi ya moyo.

Inawezekana umeshakata tamaa, baada ya kuachwa na kila mwanaume unayeanzisha naye uhusiano ukiamini una mikosi, hapo utakuwa unakosea sana, huna balaa wala nuksi ndugu yangu, ni kutojipanga na kutokuwa na utayari wa kukutana na matatizo katika uhusiano.

Hata hivyo, kwa kupitia mada hii kwa makini utaingiza kitu kipya ubongoni mwako na kukufanya uwe mpya katika ulimwengu wa mapenzi.

Kuna wengine wamekuwa wakilia kila siku, inawezekana hata wewe upo katika matatizo makubwa ya kimapenzi na huoni kama kuna sababu ya kuendelea kuishi.

Hapo unakosea sana ndugu yangu, maisha bado yanaendelea, unachotakiwa kufanya ni kujiweka tayari kukabiliana na matatizo yajayo, huku ukihakikisha kwamba huruhusu matatizo ya kujitakia katika maisha yako.




0 comments: