Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Jinsi ya kukabiliana na changamoto na hali ya kukata tamaa, ndoto zako hazikutimia bado kuna tumaini katika maisha yako..

Africa must do more to help itself; Hungry for change: a Somali woman waits for assistance as aid agencies struggle to reach drought-out hit areas; Getty


KUNA wakati maisha yako yanaporomoka kutokana na kupatwa na misukosuko ya maisha kama vile kufiwa na mke, mume au mtoto wako, kusalitiwa na marafiki uliowategemea maishani mwako, kukimbiwa na mke au mume wako, kufilisika, kupoteza kazi uliyokuwa ukiitegemea, au daktari kukuambia kuwa ugonjwa unaokusumbua si rahisi kupona.

Hali hiyo inapokutokea, unajikuta unakata tamaa ya maisha na kujiona kuwa hustahili kuishi katika dunia hii inayokuzunguka, lakini kumbuka hiyo ni njia ya kupitia katika maisha haya tunayoishi.



Hivyo ni vizuri kumtafuta rafiki yako wa karibu au kiongozi wako wa dini kwa msaada zaidi. Kwani viongozi wa dini mara nyingi wamekuwa washauri wazuri katika maisha yetu ya kila siku.

Pia ukubaliane na hali ile ambayo huwezi kuibadilisha katika maisha yako. Na kukataa kuendekeza nafsi yako katika hali ya kujisikitikia kwani hali ya kujihurumia ni ugonjwa, kama vile acid.

Hali hiyo itakuondolea hadhi yako, itakuongezea sononeko na kukata tamaa. Itakuharibia uhusiano wako na wengine. Itakusababishia hali ya kuwa na chuki. Hakuna jambo zuri litakalokujia katika maisha yako kutokana na hali hiyo ya kujisikitikia.

Usichukue maumivu yako kwa wengine. Unaporuhusu maumivu huumizi watu wengine bali unajiumiza wewe mwenyewe. Iambie nafsi yako kuwa unahusika na vitendo au tabia zako mwenyewe. Hakuna atakayeiumiza nafsi yako ila wewe mwenyewe.

Usifanye ukaidi. Kubaliana na ukweli. Si wakati wote maisha yanakuwa sawa na ya kuridhisha. Haijalishi hali inayokutokea katika maisha yako, hali ya kukata tamaa, ndoto zako hazikutimia bado kuna tumaini katika maisha yako.
Baada ya usiku inakuja siku mpya, baada ya kipindi cha baridi huja kipupwe, baada ya mvua kubwa huja jua, baada ya dhambi huja msamaha, baada ya maangamizo nafasi nyingine hutokea.


 Iambie akili yako kuwa hukuumbwa ili uwe mtu wa kushindwa.
Huwezi kuwa mtu wa kushindwa kama hujaruhusu hali hiyo katika maisha yako. Watu siku ya leo wanakata tamaa kutokana na sababu mbalimbali za maisha. Katika mtiririko wa mambo hayo, hakuna haja ya kukata tamaa katika maisha. Mtu ambaye hana kitu kinachofanya ajishughulishe anaona kuwa hana haja ya kuishi.

Kila mtu anahitaji kitu cha kushikilia fikra zake na kumpa changamoto ili kufikia malengo anayotarajia. Kumbuka, hakuna mafanikio pasipo kutaabika. Njia ya mapambano ni njia ambayo inamwezesha mtu binafsi kuongezeka, kukua, kuwa na maendeleo. Kila mtu anapitia maisha magumu kwa jinsi yake. Ni jinsi gani utakabiliana na hali hiyo ili uweze kuondokana nayo? Ni kwa kukataa hali hiyo na kusonga mbele.

Fanya jambo fulani kubwa ambalo hujawahi kulifanya kabla ya hapo. Unaweza kufanya mambo makubwa ambayo hukuwahi kuyafanya kabla ya hapo. Hiyo ni kwa sababu maumivu yako yamegeuka kuwa nyota ya mafanikio, tumia fikra zako, panua akili yako, jenga na tarajia. Uje na wazo kubwa, jambo fulani kubwa kuliko ilivyo kawaida yako. Songa mbele usikate tamaa mpaka pale matarajio yako yatakapotimia.

0 comments: