Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri
maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa
ujumla.
Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni hupunguza mtu kuwa lovable kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea direct na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni.
Kile unakula kina affect hewa unayotoa iwe mdomoni au sehemu nyingine. Na
baadhi ya vyakula vina matokeo mabaya sana kwa hurufu unayotoa mdomoni.
Harufu mbaya mdomoni si ugonjwa wa kuambukiza
haina haja kuogopa ukikutana na mtu mwenye harufu mbaya mdomoni kwamba
atakuambukiza.
Pia tatizo kubwa ni kwamba watu wenye harufu mbaya mdomoni hawajijui kwamba wana harufu mbaya. Asilimia 85 – 90% ya tatizo la harufu mbaya mdomoni asili yake ni kinywa chenyewe. Pia kiwango cha harufu hutofautiana kutokana na muda (mchana, usiku na asubuhi).
Harufu nyingi mbaya mdomoni hutokana na vyakula vyenye asilia ya protein.
Kuna zaidi ya aina 600 ya bacteria wanaoishi kwenye kinywa cha Binadamu (sehemu ya juu ya ulimi, fizi na kuzunguka meno).
NINI
HUSABABISHA KUWA NA HARUFU MBAYA MDOMONI
Kutokuwa makini na usafi wa kinywa kama vile kupiga mswaki vizuri
kunakoacha mabaki ya chakula ambayo huoza na kusababisha harufu mbaya mdomoni.
(Wengi hupiga mswaki haraka haraka na kuacha mabaki ya chakula)
Maambukizi ya magonjwa kama vile fizi kutoka damu, mfumo wa upumuaji na
kisukari. Kinywa kuwa kikavu kutokana na medications Kuvuta sigara, kunywa kahawa
JINSI
YA KUTAMBUA KWAMBA UNA HARUFU MBAYA MDOMONI
Wanasayansi wamekiri kwamba ni ngumu sana mtu kujijua mwenyewe kama ana
harufu mbaya kwa sababu ya mazoea (habituation).
Ni rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine.
Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu
unayemuamini.
Pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa,
wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa.
Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa.
Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama Halimeter, Gas Chromatography na
BANA Test.
JINSI
YA KUJILINDA NA HARUFU MBAYA MDOMONI (TIBA)
Kula vyakula vyenye afya na pia kula vyakula ambavyo wakati unakula
vinaweza kusafisha kinywa vizuri.
Kusafisha meno mara mbili kwa siku asubuhi na baada ya mlo wa usiku,
unashauriwa kutumia tongue cleaner kusafisha ulimi.
Tumia chewing gum ambazo husaidia kuongeza kiasi cha mate kwenye kimywa
kilichokauka. Baadhi ya gums zina viungo vinavyoondoa harufu mbaya mdomoni na
zingine husafisha kinywa na bacteria wanaosababisha harufu mbaya.
Tumia dawa ya kusukutua mdomoni (mouthwash) kabla ya kulala usiku.
Kuwa makini na afya ya kinywa chako kama vile kupiga mswaki vizuri,
kuondoa mabaki ya vyakula kwenye meno na kumuona daktari kila unapoona una
Matatizo ya meno au kinywa.
Kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku angalau glass mbili za
maji.
0 comments: