Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Porojo na Umbea umeshakuwa mitaji ya watu hapa kwetu.. Soma hapa kwa undani wake..!!




Porojo na Umbea inaweza kufanya maisha yako yaonekane kama sinema. Karibu kila siku unaweza ukasikia porojo kukuhusu wewe, uvumi kwamba una mimba, umetoa mimba mara kadhaa, ama ni mlanguzi wa dawa za kulevya  na wewe hutumia dawa za kulevya. Watu wanasema mambo kama hayo kukuhusu?
Mvulana au msichana mwenye nia mbaya anaweza kukuharibia sifa yako akitumia barua-pepe na ujumbe mfupi pasipo hata kufumbua kinywa chake. Uvumi mbaya sana unaweza kuenea haraka kwa kuandika maneno machache tu na kuyasambaza! Katika visa fulani, wengine wameanzisha tovuti (Web site) ili kumwaibisha mtu fulani. Kwa kawaida blogu kwenye Intaneti huwa na porojo chungu nzima ambazo mtu hasingeweza kuzisema uso kwa uso.

Hakuna shaka kwamba maneno yanaweza kuumiza. Ndiyo sababu unapaswa kupima maneno yako! Ni kweli kwamba baada ya mazungumzo kupamba moto ujasiri unahitajika ili kuyakatiza. Unahitaji kuwa mwangalifu unasema nini. Ikiwa hujasikia jambo kutoka chanzo kinachotegemeka, huenda ukawa unaeneza uwongo.” Kwa hiyo, unaposikia mambo yanayoweza kugeuka na kuwa porojo yenye kudhuru, 

Unaweza kufanya nini porojo ikienezwa kukuhusu? Usiwe na haraka kuudhika katika roho yako.” Badala yake, jaribu kuzuia hisia zako na kutochukua mambo kwa uzito kupita kiasi. 

Usiweke moyoni mwako maneno yote ambayo huenda watu wakasema, kwa maana moyo wako mwenyewe unajua vema kwamba hata mara nyingi wewe, umewalaani wengine.

Basi, tenda kwa hekima kwa kubadili mazungumzo yanapoanza kuwa porojo yenye kudhuru. Na mambo mabaya yanaposemwa kukuhusu, onyesho ukomavu kwa kutoachilia hisia zikuongoze. Acha ujulikane kwa matendo yako mema.

0 comments: