Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Je..!!! Una kipato kidogo lakini Matumizi makubwa..? Jifunze hapa namna ya kutumia Kipato hicho na kutosheleza Mahitaji yako..



Watu wengi husindwa kubana matumizi kutokana na kukosa elimu ya jinsi ya kutumia pesa. Baadhi wamesoma na wengine wanaendelea kusoma masomo mbalimbali yanayohusu pesa na wanahitimu vizuri, lakini wanapokuja katika uhalisia wa maisha wanajikuta wanafeli vibaya kutokana na kutoutambua umuhimu wa kuwa na nidhamu ya pesa.

Msomaji wangu nikupe dondoo kadhaa ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kukusaidia katika kubana matumizi na hatimaye hata kama kipato chako ni kidogo, kikakidhi mahitaji yako muhimu na pia kukawepo na ziada.



Usipendelee kukopa

Kuna watu wengi sana wanaishi kwa kukopa kopa vitu madukani na kwa watu. Mtindo huu ni mbaya sana kwa ukadiriaji wa matumizi, kwani haumtii uchungu mkopaji hadi pale atakapokuwa analipa. Mara nyingi ukopaji huongeza gharama, hivyo inashauriwa ukiwa na 5,000 itumie hiyo, bila kutafuta ziada kwenye deni.

Kuwa na bajeti ndogo

Katika maisha pendelea kupanga bajeti yako kwa mafungu madogo madogo hasa ya wiki. Usivuke mipango hiyo kwa kutumia bajeti ya wiki inayofuata.

Usitembee na pesa nyingi

Baadhi ya watu wanapenda kutembea mitaani huku wakiwa na pesa nyingi mifukoni. Fahamu kuwa kutembea na pesa usizozipangia bajeti utajikuta unashawishiwa kuzitumia bila mpango.

Hata hivyo, unashauriwa kujenga tabia ya kukaa nyumbani na familia yako na kama utatoka siku za mwisho wa wiki basi weka bajeti ya kiasi ambacho utakitumia. Kitendo cha kutoka huku ukiwa na fedha nyingi kwenye pochi lako ni kujishawishi kufanya matanuzi yasio na msingi.

Epuka kununua vitu kwa rejareja!

Unapopata mshaara wako au unapofikiria kuhusu matumizi ya nyumbani kwako pendelea sana kununua vitu kwa jumla ambavyo utavitumia kwa mwezi mzima. Epuka kununua vipimo vidogo vidogo kwani vinaumiza na kuvuruga bajeti.

Pika chakula nyumbani kwako

Watu wengi hasa vijana wanapenda sana kula kwenye migahawa na hotelini. Ulaji huu ni ghali, hivyo inashauriwa kila mtu ajipikie chakula chake nyumbani. Hii itamsaidia kutumia pesa kidogo katika suala la chakula.

Ifundishe familia nidhamu ya pesa

Kuna watu hawawafundishi watoto na wake zao nidhamu ya matumizi ya pesa. Mume/mke asinunue vitu ambavyo familioa haikuzitengea bajeti na asiwepo mtumia hovyo vitu vilivyonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Akiba na mipango ni muhimu

Familia lazima ijiwekee akiba benki. Utunzaji wa pesa nyumbani si wa salama na mara nyingi hushawishi matumizi. Aidha unapoweka feda benki ziwekee malengo amambo utakuwa ukiyatimiza taratibu si mpaka pesa hizo ziwe nyini.

Kuwa na familia ndogo

Ingawa ni hali halisi ya maisha ya kiafrika kwa familia moja kuwa na watu wengi lakini inashauriwa kwamba, ili kupata ziada ya kipato lazima familia iwe ndogo, vinginevyo mshahara wote unaweza kutumika kwa chakula tu. La kama familia itakuwa ni kubwa basi kila mmoja afanye kazi ili uwepo usaidianaji wa kuendesha familia.


Punguza Matumizi ya Vocha kwenye Simu

Weka vocha una wasiliana na mtu mwenye shida nae lakini sasa watu wamekuwa wakijiunga na massage kila siku kwa ajiri ya kuchati tu lakini hawajui kiasi gani wanapoteza kwa kila mwezi. Piga mahesabu leo ujue unatumia kiasi gani kwa mwezi kama vocha na je hao unao wasiliana nao ni wana umuhimu kweli.

Chukua hatua........

0 comments: