Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Kujihurumia wakati wa Matatizo Unaporuhusu hali hiyo kuondoka, mafanikio yako yataonekana.. Soma zaid hapa...



Hali hiyo ya kujihurumia  inakurudisha nyuma kimaendeleo. Unaporuhusu hali hiyo kuondoka, mafanikio yako yataonekana. Kumbuka kila mara unapojionea huruma hakuna chochote utakachoweza kukifanya. Kusikitika si njia ya kukufanya ujisikie vizuri.
Je, wataka mambo yako yawe mazuri? Chukua hatua zifuatazo. Jiulize mwenyewe hali hiyo imefanya jambo lolote zuri kwako?

Je, imebadilisha mambo yaliyokutokea? Hapana. Je, hali hiyo imebadilisha mambo mabaya yaliyokutokea kuwa mazuri? Hapana. Je, hali hiyo imekufanya ujisikie vizuri?

Je, hali hiyo imekufanya kupendwa? Je, hali hiyo imekujengea mapenzi na heshima? Je, hali hii imeniletea mafanikio na uhodari? Je, hali hiyo imekuweka karibu na wengine? Je, hali hiyo imekuongezea kupendwa na wengine? Je, hali hiyo imekujengea uwezo? Je hali hiyo imekuponyesha majeraha uliyoyapata? Je, hali hiyo imekuwezesha kuelewana na wenzako?

Hata iweje, hali hiyo haiwezi kukuongezea kitu zaidi ya kukuzidishia maumivu na kukufanya mnyonge. Kama unataka kuendelea kuwa na huzuni, kuwa na masononeko, kutokuwa na marafiki, kuwa mgonjwa, kuwa na matatizo ya mara kwa mara, hivyo endelea kujisikitikia lakini kama unataka kujisikia kuwa na maisha mazuri amua kuachana na hali hiyo.

Ili kuondokana na hali hiyo yakubidi ufanye yafuatayo:

Kwanza, yakupasa uigundue hali hiyo haraka na baini kilichosababisha hali hiyo. Hali ya ubinafsi inasababisha kuwa katika hali ya kujisikitikia.
Kuona kila kitu kinakwenda vibaya na hakuna hata kimoja kilicho sahihi. Jitahidi kuondokana na hali hiyo itakuongezea majuto.

Pima uwezo wako kupambana na hali hiyo kwa kuchagua kipi bora zaidi ya hali inayokukabili. Haijalishi ni hali gani unayokumbana nayo, cha msingi ni kuikataa hali ile inayokufanya kuwa mnyonge au kujisikitikia.

Fanya mazoezi ya viungo. Mazoezi ya viungo yana faida kwa maisha ya mwanadamu. Mfano kuna baba mmoja alifiwa na mke wake. Anasema alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa asijue la kufanya, ndipo alipotokea rafiki yake ambaye alitaka kumsaidia.

Alizungumza naye juu ya kujiunga na sehemu ya kufanyia mazoezi ya viungo ambapo alikuwa akimpitia kwa wiki mara tatu na kumpeleka sehemu hiyo.
Anasema rafiki huyo alimsaidia sana kwa kuwa aliacha kuwaza juu ya matatizo yaliyomkuta. Mwili wake ulianza kuimarika, kubadilika na kujengeka upya. Anasema mazoezi hayo yalimfanya mwili wake uchoke na kupata usingizi usiku alipolala.

Jambo jingine, tarajia maumivu fulani ya moyo wakati wa zoezi hilo. Kumbuka ni juhudi zinazomfanya mtu awe na nguvu. Ni mambo magumu yanayomfanya mtu abadilike. Pia ni vikwazo vinavyomfanya mtu apate changamoto kubwa na fursa nzuri.

Ni vizuri kuwekeza mawazo au malengo yako yote kwa kile ukipendacho, si kwa kile ulichopoteza. Watu wengi hupatwa na maumivu kwa kuwa wamesimamia katika upungufu wao, kupoteza na vikwazo wanavyokutana navyo. Hilo ni tatizo kubwa kwa watu wengi.

Jitolee kuwahudumia wengine. Njia mojawapo ya kuondokana na hali hiyo ni kwenda kuwatembelea ndugu, jamaa na marafiki majumbani kwao. Unapofanya hivyo unajikuta unasahau mambo yaliyokupata.

Usiwe katika hali ya kujihurumia unapopatwa na matatizo ili usiache nafasi ya wengine kukuhurumia..

0 comments: