Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Ona jinsi Ndugu, jamaa na marafiki wanavyo weza kukufilishi katika biashara yako..

Shops


Biashara inatunzwa na Mfanya biashara na kuzalisha mapato. Katika mapato hayo mfanyabiashara anajilipa mshahara kutokana na kupata faida. Mshahara anao jilipa ndounatumika kwa matumizi binafisi ikiwemo kutunza familia. 

Katika hili ni vyema fedha ya Biashara na ya familia itengwe ili kuepuka mwingiliano wa matumizi. Ili biashara iweze kukua vizuri ni lazima mfanya biashara aelewe namna ya kutenga fedha ya biashara na ya familia

Biashara ina nafasi kisheria kama binadamu, na inalindwa na sheria na ndiyo maanainapewa jina na kusajiliwa. Kwa kua biashara na mwenye biashara ni vitu viwili tofauti na matumizi yao ni tofauti pia. Kwa hiyo fedha ya biashara ni ya biashara na ya familia ni ya familia, vitu hivi viwili havi changwanywi.

NJIA ZAKUBADILISHA FAMILIA IWEZE KUISAIDIA BIASHARA KUIMARIKA NA KUKUA

1. Elimisha famila yako maana na umuhimu wa biashara yako katika kuendeleza familia hiyo. Biashara ndiyo inayo itunza familia . Ili biashara iweze kuitunza familia nilazima itunzwe vizuri. Mfano Jinsi ng'ombe anavyo tunzwa vizuri ndivyo anavyotoa maziwa mengi. Yale maziwa yanauzwa na kulipa ada za shule na kazalika.

2. Wape elimu yabiashara ili wakusaidie kusimamia biashara yako
3. Usiajiri wanafamilia ambao si waaminifu
4. Washirikishe wana familiakatika kuzalisha na si katika matumizi tu
5. Kuwa muwazi na mkweli kwa familia yako kuhusu kipato halali kinachopatikana kwenye biashara yako

ATHARI ZA KUENDEKEZA UNDUGU, UJIRANI, URAFIKI KATIKA BIASHARA

1. Uzoefuunaonyesha kwamba ndugu na marafiki wakikopa hawarudishi, Na wakijua kuwa wewe ni rahisi kutoa misaada basi kuomba hakuishi na matokeo yake ni.
- Kujenga uadui wakati unapo kuwa huwezikuwasaidia
- Kudhoofisha biasharayako kwa kutoa misaada mingi sana
- Kuathiri maendeleo yafamilia yako
- Kushindwa kulipamikopo uliyo chukua
- Kufilisika

NJIA ZAKUELIMISHA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI
1.Waelimishe wasaidie biashara yako kukua vizuri badala ya kuiharibu
2. Unaweza kuwaelimishakwa kuongea nao wewe mwenyewe ana kwa ana
3. Unaweza tumia mtaalaau mtu mwingine atakaye weza kuwaelimisha vizuri

0 comments: