MAMBO
YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI
Hakuna
njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
1. Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi
kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu
,usikwaruze kwa kucha au kitu choichote kigumu.
2. Tumia make-up au vilainisha ngozi visivyo na
mafuta mgando
3. Osha nywele zako kila mara na epuka nywele
kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
4. Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye
mafuta mengi.
5. Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu
chenye ncha kali.
6. Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni
mzuri ili kupata vitamin D
DAWAZA
KUMEZA
Wakati
mwingine daktari anaweza kumshauri mgonjwa kutumia dawa za kumeza kulingana na
wingi au ukubwa wa tatizo.
Dawa
kama antibiotics huua wadudu na huzuia chunusi ,dawa hizo ni kama vile
Erythromycin topical, Accutane (isotret-inoin), Benzamycin Cleocin T
(clindamycin phosphate), Desquam-E (benzoyl peroxide) Minocin (minocycline
hydrochloride)
DAWA ZA
KUPAKA
Kuna
dawa za kupaka ambazo hupaka katika eneo la ngozi lililoathirika kwa chunusi.
Dawa hizi hupatikana kama cream,lotion,gel au pad. Dawa hizi hutumika kutibu
chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo
tu.
Mojawapo
ya dawa hizi ni antibi-otic kama zenye mchanganyiko wa gentamyicin na
betamethasone au dexame-thasone kama vile Gentrisone au Gentriderm
cream,Erythromycin,B-Tex na kadhalika.Pia Persol forte Gel husaidia hasa
ukianza na asilimia ndogo (2.5%) na kuendelea kadri ngozi yako inavyohimili
dawa.
MATIBABU
MENGINE
Kwa
nchi zilizoendelea matibabu yanaweza kuwa hata upasuaji mdogo (skin grafting)
au plastic surgery kama chunusi imesaba-bisha baka kubwa na kuna njia kama vile
Chemical peel ambapo kemikali hupakwa kwenye ngozi na inapokauka kipande au
gamba la juu la ngozi huondolewa na kuondoa baka.
0 comments: