Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Ukichunguza kwa makini watoto mbumbumbu darasani ni wale ambao wazazi wao hawakuzingatia mambo yafuatayo...!! Soma hapa

Yourng girl doing homework with her mother

Ukichunguza kwa makini watoto wengi wanaokuwa mbumbumbu darasani (nazungumzia wale wasiokuwa na kasoro za kibaiolojia) ni wale ambao wazazi wao hawakuzingatia mambo yafuatayo katika kuwalea tangu walipokuwa wadogo hadi kukua kwao.


HUDUMA BORA
Wazazi wengi hasa wa dunia ya tatu wanakabiliwa na tatizo la uzazi holela, usiozingatia uwezo wa kulea na kuwapatoa huduma muhimu kwa watoto. Mfano lishe bora, mavazi na malazi.

 Wanasayansi wanasema chakula bora ndicho kinachoweza kuimarisha ukuaji wa viungo vya mtoto na kuufanya ubongo uwe katika hali nzuri ya kumudu kutafsiri mambo.

Hivyo ni jukumu la mzazi anayetaka mtoto wake awe na uelewa mzuri darasani ahakikishe kuwa anampatia mwanae chakula bora kitakachomjenga afya na kumuwezesha kuwa na mwili wenye nguvu ya kukabili magonjwa ya kitoto.

Lakini sambamba na hilo mzazi anatakiwa kusimamia afya ya mwanae kwa kumpeleka hospitalini mara kwa mara kutibiwa na kushauriwa.

UTAMBUZI WA KIPAJI
Jambo la pili ambalo ni muhimu kwa mzazi ni kutambua mapema kipaji ha mtoto na kumuongoza sawa na kipaji chake. Ingawa shule nyingi nchini (Tanzania) hazitoi elimu ya ngazi ya chini lakini baba na mama bado wanawajibika kujua ni elimu ya kiwango gani kutoka shule gani itamfaa mtoto wao.

Inashauri kwa mzazi kumtambua mwanae ana uelewa gani, ili ajue namna ya kumsaidia ili afikie kiwango bora cha uelewa. Kwa mfano mtoto akiwa na uelewa wa chini anatakiwa kupelekwe kwa waalimu wazuri wenye uwezo wa kumsaidia anaposhindwa, haifai mtoto wa aina hii kupelekwa shule za ilimradi na kudhani huko atasoma na kuelewa.

0 comments: