Ni
watu wachache wanaofahamu umuhimu wa kuwa na rafiki katika maisha yao. Wengi
kati yao wanajikuta katika makundi ya watu bila kujua faida ya kuwa na
ushirikiano na wengine.
Uelewa
mdogo wa wazazi/walezi umewafikisha katika hatua ya kuwazuia watoto wao
kutembelewa na marafiki zao nyumbani na hivyo kuamua kuwafungia ndani ya geti
kila wanapotoka shule kwa hofu kuwa marafiki watawaharibu tabia watoto wao.
Inawezeakana
wazazi wakawa sahihi endapo tu marafiki wanaoambatana na watoto wao ni wabaya,
lakini mtoto kuwa na rafiki mwenye akili darasani, adabu na ufahamu mkubwa ni
jambo muhimu ambalo linafaida nyingi katika kusaidia malezi yake.
Neno
rafiki huwezi kulitofautisha na Upendo, kwa kuwa tafsiri inayopatikana katika
Kamusi ya Kiswahili Sanifu inabainisha ni 'Kupendana na kuaminiana na
mwingine'. Hivyo basi kumzuia mtoto asipendane na kuaminiana na mwenzake ni
kumdumaza akili.
Uchunguzi
unaonesha kuwa baadhi ya wazazi nao si rafiki wema kwa watoto wao kwa maana ile
ya kamusi ya kupendana na kuaminiana. Lakini wengi wao wanaishi kwa desturi
iliyotokana na uzazi tu. Upo ushahidi mwingi juu ya wazazi ambao wanaishi na
watoto wao kama marafiki wabaya wakiwakosea adabu na kuwafundisha mambo ya
kihuni.
Kama
hilo halitoshi watoto hasa wanaosoma shule, mara nyingi wamekosa msaada wa
kirafiki kutoka kwa wazazi wao kutokana na watu wanaoishi nao kuwa katika
masumbufu ya dunia kupita kiasi au wakati mwingine ukali uliopindukia, jambao
ambalo huwafanya watoto waishi ndani ya familia kama watumwa na hivyo kuwa na
kiu ya kufarijiwa na watu wengine ambao ndiyo marafiki tunaozungumzia habari
zao.
Kwa
maana hiyo ili mwanafunzi/mwanadamu wa kawaida afikie kilele cha furaha, lazima
awe na marafiki wa kupendana nao (simaanishi wapenzi wa kingono). Hawa ndiyo
watakaomfariji atakapokuwa na msongo wa mawazo, watakaomfanya acheke,
watakaomshauri, watakaomsukuma awe mtu mwema.
Ni
wazi kwamba mtoto hawezi kufahamu mambo ya ulimwengu kwa kufungiwa ndani na
mara nyingine kufanya hivyo ni kujaribu kuzuia jambo ambalo halizuiliki katika
ulimwengu huu wa utandawazi.
0 comments: