Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Tabia za wanafunzi wawapo shuleni ni kutekwa akili zao bila wao wenyewe kujua kwa kufuata tabia za kimakundi.. Soma hapa



Uchunguzi unaonyesha kwamba wanafunzi wengi hubadilika kitabia wanapokuwa masomoni. Hii ina maana kuwa wazazi wanaweza kujitahidi kumuandaa mtoto wao lakini wakajikuta wanapata matokea ambayo hawakuyatarajia.


Jambo kubwa ambalo huathiri tabia za wanafunzi wawapo shuleni ni kutekwa akili zao bila wao wenyewe kujua kwa kufuata tabia za kimakundi au kwa lugha ya kigeni Mob- psychology.

Inawezekana kabisa mwanafunzi akatoka nyumbani na kujiunga na shule fulani akiwa mtu safi mwenye akili darasani, lakini baadaye akajikuta anabadilika kidogo kidogo na kufikia hatua ya kuwa muhuni na hata mtumiaji wa dawa za kulevya au malaya na hatimaye kushindwa masomo.

Hivyo, ni wajibu wa mwanafunzi mwenyewe kuwa makini na mvuto wa kimakundi atakaoukuta shuleni na kujihadhari. Inashauriwa kuwa si busara kuiga kila jambo linalofanywa na wengine kwa msukumo wa nje, mfano kuona aibu kwa kuitwa mshamba.

Si vema kujiunga na makundi kufanya jambo fulani bila kutafakari kwa kina faida na hasara. Ni muhimu kwa mwanafunzi kusimamia jambo analoliamini na kutokukubali kubadilika kirahisi kwa kushawishiwa au kuzongwa na kauli za wengi.

0 comments: