Juhudi
katika utafutaji wa kipato.
Kutokana na mahitaji kuongezeka katika miaka ya karibuni,inalazimu mwanaume na
mwanamke wote kwa pamoja washiriki katika kujiongezea kipato ili kujitosheleza walau kwa mambo
muhimu ya kila siku. Kiukweli ni nzuri sana kwa mwanamke kuepukana na hari ya
utegemezi kwa kiasi kikubwa, Hii itajenga upendo wenye heshima na itamwongezea
mwanaume kutambua umuhimu wa uwepo wa mwanamke umuhimu ambao ni adimu sana
kuupata hasa kwa jamii za kiafrika.
Maarifa
juu ya mapenzi na tendo la ndoa.
Mapenzi na tendo la ndoa ni vitu tofauti japokua tendo la ndoa ni kipengere
mojawapo katika mapenzi.Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha mwenziwake
anafurahia mapenzi yenu ima kwa kujariana,kushauriana,kusikili zana na
kuheshimiana.Linapokuja swala la tendo la ndoa ni wajibu wa kila mmoja
kuhakikisha anajua ashughulike vipi ili kutoshelezana.Mambo haya ni muhimu sana
katika tendo la ndoa
i- Kuandaana kisaikolojia kabla ya tendo la ndoa kwa mfano;kutumiana meseji endapo mpo mbali kidogo,kusuluhisha kama kuna mgogoro.
ii- Kuzijua sehemu za hisia za mwili wa mwenzi wako (sehemu za mwanamke zipo 12 na kwamwanaume zipo 5)
iii- Unadhifu na Usafi wa mwili kabla ya tendo la ndoa.
iv- Ushirikiano wapamoja wakati wa tendo la ndoa,Mfano;Mikao(style) ambayo italeta hari ya hisia zaidi, Mideko na kilio cha wastani toka kwa mwanamke humuhamasisha zaidi mwaume, kubembelezana na lugha za upole.
Urafiki
wa karibu zaidi. Unaweza
ukawa na ndugu yako au mpenzi wako lakini asiwe rafiki yako.Urafiki ni hari ya
kushirikishana mambo mengi pamoja naya siri binafsi. Kwaiyo,mfanye mwenza wako
awe rafiki yako 100%. Mshirikishe mwenzako mambo yote yanayokusibu, mfanye awe
mshauri na mfariji wako ni jambo ambalo litamfanya ajisikie fahari kuwa na wewe
kwa kutambua uwepo wake.
Utu. Jijengee hari ya usawa
kwa mwenzako.Mfanyie mwenzako ambayo hta wewe ungependa akufanyie.Ifanye akiri
yako iijengee roho yako mazingira ya kua upendo na jamii inayokuzunguka. Kua
mwepesi wa kusaidia,kushirikiana na kujari wanajamii wenzako. Jamii inapotambua
mchango wako ni dhahiri utasifika na kuheshimika. Hivyo utamfanya mwenzako
akupende zaidi na kuiga mfano toka kwako.
Ukweli
na uwazi. Huu
ni msingi wa uaminifu katika kukuza upendo wa mwenzako.Uwongo hubeba tabia
zilizojificha ndani yake (eg:Dharau,kiburi,Unafiki)
. Jitahidi kuwa mkweli kwa mwezako,kama kuna jambo hupendezwi nalo kuwa muwazi
umweleze kwa lugha ya upendo. Usithubutu kuwa msiri katika mapenzi. Mnapokuwa
faragha mueleze mwenzako hisia zako. Unapoona tatizo kuwa wa kwanza kushiriki
katika utatuzi.
Imani
za kidini. Jifunze
kuwa na maadiri mema.Jitahidi kushika mafundisho mema ya dini yako hususani
wakristo na waislamu wote tunafundishwa kutoka nje ya ndoa ni dhambi mbele za
mwenyezi Mungu. Kwahiyo,Imani yako imara itakufanya umuogope muumba wako na
itakuepusha dhidi ya fikra potofu za usaliti. Pia itakurahisishia kujenga
familia nzuri yenye furaha,amani na upendo.
0 comments: