Imebainika kwamba, wanaume wanaposaka wapenzi, huwa tayari kutii masharti wanayopewa na upande wa pili. Utii huu ndiyo unaotajwa kumvutia mwanawake kiasi cha kumfanya kuaamini kirahisi kuwa mwanaume wa maisha yake ni huyo anayemtongoza wakati huo.
Hakuna shaka kwamba, katika mazungumzo ya awali ya mwanaume anayemteka mwanamke kimahaba, kinywa chake huwa hakikauki maneno haya manne zenye nguvu ya kumdatisha mwanamke, ambazo ni NAKUPENDA, NAKUHITAJI, SAMAHANI na ASANTE.
Ni wazi kwamba kuna wanaume wengi ambao huanza na gia kubwa ya maneno hao
wamebainika kupoteza mvuto wa kimapenzi waliokuwa nao mwanzo kwa wapenzi wao.
Kama nilivyosema neno la
kwanza lenye nguvu ya kumteka kimapenzi mwanamke ni NAKUPENDA. Neno hili ni
tiba inayoponya hofu na kumfanya mwanamke ajiamini.
Neno la pili, NAKUHITAJI. Kama inavyokuwa wakati wa kutongoza, mwanamke anapenda kuambiwa neno hilo na kufanyiwa vitendo inavyoonesha kuhitajika kwake katika maamuzi, matembezi, faraja na muongozo wa kimaisha. Sambamba na hilo mwanamke anapenda sana kupewa ASANTE katika yale anayofanya.
Jambo la mwisho kabisa ni SAMAHANI. Ndugu zangu kuna wanaume ambao hawako tayari kuomba msamaha kabisa hata kama wamekosa kosa kubwa na la wazi kiasi gani? Kifupi tabia hiyo haipendezi. Ni busara kwa mwanaume kumuomba radhi mpenzi wake, ili naye ajione ni mwenye mamlaka na hivyo kuzidisha upendo na uangalizi wa tabia mbaya za mwanaume.
Kila
la heri katika mapenzi yako………
0 comments: