Ukosefu
wa nguvu za kiume nchini twaweza kusema
ni janga. Hii ni kutokana na tafiti zilizowahi kufanywa na pia kuzagaa
kwa vibao vya matangazo kuhusu dawa au tiba ya tatizo hilo.
Sababu
nyingi zimewahi kuanishwa kuchochea ugumba kwa wanaume ikiwamo maradhi,
kutazama luninga kwa muda mrefu na kutofanya mazoezi. Zifuatazo ni baadhi ya
vitu vinavyosababisha tatizo hilo;
Madereva, Dk Kava
anasema wakati wa zama za chuma ilibainika kwamba wanaume wanaoendesha baiskeli
kwa muda mrefu, waendesha farasi na madereva wa magari kwa muda mrefu wamo
hatarini kukosa nguvu za kiume.
Jarida
la tiba lilifanya utafiti na kubaini kuwa asilimia nne ya wanaume wanaoendesha
baiskeli kwa saa tatu au zaidi kwa wiki wanapata matatizo ya nguvu za kiume.
Anasema
unapokaa kwenye gari, farasi au baiskeli kwa muda mmrefu unaweka nguvu katika
neva na mishipa midogo inayobeba damu kwenda katika uume. Anafafanua kwamba
uendeshaji wa vyombo hivyo kwa muda mrefu unaharibu mishipa midogo na damu
haiendi inavyotakiwa katika uume.
Maradhi ya fizi, Pengine
unaweza kujiuliza fizi na nguvu za kiume vina uhusiano gani? Wataalamu wa Afya
wanasema, kuwa na matatizo sugu ya fizi au fizi zilizoathirika kunaweza kuongeza
hatari ya mtu kukosa nguvu za kiume. Watafiti
wanasema maradhi ya fizi ni dalili za afya dhaifu na inahusishwa na ongezeko la
maradhi ya moyo na upungufu wa nguvu a kiume.
“Maradhi
ya fizi yanaweza kusababisha matatizo katika kusukuma damu, hivyo matatizo hayo
yakizidi, yanaweza kusababisha damu ishindwe kufika katika uume,”
Msongo wa
Mawazo,
Pia asilimia 61 ya watu wenye msongo wa mawazo hawawezi kuwa na nguvu za kiume.
Taarifa kutoka Kliniki ya Cleveland inaeleza kwamba msongo wa mawazo
unasababisha mambo makubwa zaidi katika mwili na unaweza kuathiri kwa kiasi
kikubwa nguvu za kiume.
Msongo
wa mawazo unasababisha Kemikali za seli za ubongo zinazowasiliana katika
kusisimua mtiririko wa damu hadi katika uume kushindwa kufanya kazi. Pia Dk
Malebo anasema wanaume hukosa nguvu za kiume kutokana na msongo wa mawazo ambao unatokana na migogoro ya kifamilia,
ufukara au imani za kishirikina.
Aina za
vyakula, mtindo wa maisha, msongo wa mawazo na utofauti katika vichocheo ni
baadhi tu ya sababu za ukosefu wa nguvu za kiume.
“Baadhi
ya vyakula vina kemikali ambazo zinapoingia katika mwili zinaharibu usukumwaji
wa damu katika uume”
Samaki na
maziwa,
ni sababu Kwa mfano, watu wengi hununua maziwa ya ng’ombe ambayo yamechomwa
sindano siku mbili au moja nyuma bila wao kufahamu
“Au
samaki wanaovuliwa kwa kemikali na mabomu ni sababu zinazochangia kwa kiasi
kikubwa ukosefu wa nguvu za kiume,” anasema. kemikali hizo zinaathiri
uzalishaji wa vichocheo na usukumwaji wa damu kutoka katika moyo hadi katika
uume.
Ushauri na
tiba
Anashauri kuwa ili kuepukana na tatizo la nguvu za
kiume hasa kwa wale wenye msongo wa
mawazo sulushisho ni kubadili mfumo wa maisha.
“Kuhusu
mvurugiko wa homoni, udhibiti wa serikali unahitajika. Maziwa ya ng’ombe,
yanayokamuliwa wakati ng’ombe amechomwa sindano pamoja kemikali za kuvulia
samaki zidhibitiwe,”
Anasema
uwiano mbovu wa vichocheo unaweza kutibika hospitali kwa dawa zinazorekebisha
mfumo huo na pia zipo dawa za asili.
Mmea
wa Alikisusi (licorice) kwa kisayansi Glycyrrhiza Giabra una uwezo wa
kutengeneza uwiano wa vichocheo kwa wanaume wenye matatizo ya nguvu za kiume.
0 comments: