Kuna maneno
mengi hutokea na kuwepo pale wawili wanapopendana. Upendo ni kitu ambacho
hakizuiliki. Napale patakaposhikilia ule upendo ipasavyo ndo husikii wala huoni
utakaloambiwa juu ya akupendaye. Matendo mbalimbali yanayofanywa na wale
wapenzi moja kwa moja huchochea upendo wa moyoni ambao hudumu milele, ndio hapo
utasikia keshapewa madawa, mara mke wake kamkalia kila atakachoomba lazima
apewe namengine mengi ambayo umekumbana nayo au kuyashuhudia kwa watu
wengine.
Moja kwa moja niende kwenye hivo vichochezi kama ifuatavyo:
• Kusikiliza na kua mshauri mwema kwa mwenzako.Iwe
ni kuhusu familia yake au mipango yake ya baadae au kimasomo,kikazi na hata
kibiashara.Ikumbukwe kuwa mafanikio ya mmoja ni chachu ya maendeleo mazuri
hata mtakapokua katika familia.
• Kujishusha panapotokea kutokuelewana (yaani kuwa
mwepesi wa kuomba msamaha).Majibizano siku zote hayajengi hasa mnapokua mna
hasira au mmoja kati yenu ana hasira.
• Neno ahsante ni dogo sana ila lina couragement
kubwa saana, Ukipongezwa na hata unapopewa pole shukuru. Unapopewa chochote na
mwenzako iwe ni ushauri, maoni, mawazo mapya juu ya miradi mbalimbali au kazi
huna budi kushukuru.
• Mwepesi wa kusamehe na kusahau.Vilevile mwelekeze
mwenzako pale alipokosea ili siku nyingine kitendo hicho kisitokee.Usiwe
mwombaji mzuri wa msamaha huku wewe hautoi.
• Msifie mwenzako anapopiga hatua ya maisha anapokua
katika muonekano mzuri n.k Usisubiri jirani amwambie. Tena hapa muwe makini
sana maana ni rahisi kwa mwingine kuvutika upande wa pili kwa ajili
yakusifiwa(Kusifia kunajenga picha ya kujali) japokua sio wote
wanamaanisha.
• Kuwa mkweli na mwaminifu katika mahusiano yenu
• Usisubiri matukio maalum ndo utoe zawadi kama vile
birthday,valentine day n.k,Mpe wakati wowote unapokua na uwezo wakumpa.
• Usimuulize mpenzio anataka zawadi gani.Siku zote
zawadi ni kitu ambacho mpokeaji hakijui na wala hatakiwi kukijua kabla
hujampelekea.Kuna zawadi nyiingi sana ambazo unaweza mpa mwenza.Na kupitia muda
wa urafiki wenu naamini utaweza kujua walau nusu kama si robo tatu ya vitu
anavyovipenda.Ila jitahidi uwe ni muibuaji wa vitu vipya sio vilivyozoeleka.
Natumaini
kwa kiasi Fulani vitu kama hivyo kutoka kwa mwenza wako vimekufanya au
vinakufanya umpende zaidi.Au ukosaji wa vitu hivi kwa mwenzako vimekufanya
mshindwe kuendelea kua katika mahusiano au kuvunjika moyo.Jiheshimu na pia
muheshimu mwenzako pamoja na hisia zake,mjali,mthamini,mtie
moyo,mrekebishe anapofanya ndivyo sivyo na lingine ni kuombeana Baraka za
mwenyezi Mungu zikae nanyi nakuwaongoza katika kila jambo.
0 comments: