Matatizo mengine kutajwa
kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni
mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye
mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.
Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa
masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo vina
uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa.Vyakula hivyo ni hivi
vifuatavyo:-
1.PILIPILI. Pilipili zilizocheshwa
zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini, ambao
kwa kiasi kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya mtu akawa na hisia kali za kimapenzi.
Kwa msingi huo, ni vema kwa wale wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya
mapenzi wakatumia pilipili si kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe
hisia zao.
2.PARACHICHI. Aina nyingine ya chakula
ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi.
Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika
uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana
msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongezamajimaji
yenye utelezisehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa
kujamiiana.
3.NDIZI. Wakati unafikiria uwezo wa
kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili
ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa
msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na
kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.
4.CHOKOLETI. Ulaji wa Chokoleti huongeza
uchangamfu mwilini na, hivyo kumuwezesha mtu anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na
mguso sahihi kwenye fikra zake, jambo litakalomuwezesha kupokea hisia za
mapenzi kwa urahisi zaidi ya mtu ambaye anakwenda kwenye uwanja wa sita kwa
sita akiwa mchovu wa mawazo.
5.CHAZA NA PWEZA. Aina hizi za samaki zinazovuliwa
baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa
vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.
6.POMEGRANATE. Ni aina fulani ya
matundamekundu yanayofananana na apple. Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa
ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo
kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.
7.MVINYO MWEKUNDU. Mvivyo mwenyekundu unatajwa
kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha
kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu
kunywewa hasa na wale ambao wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia
tendo.
8.MBEGU ZA MATUNDA. Mchangayiko wa mbegu mbalimbali
za matunda, mfano tikiti, maboga husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu
ajione ni mwenye afya njema.
9.VANILLA. Vanila husaidia kuamasha hamasa
mwili.
10.TIKITIMAJI. Ambalo linatajwa kuwa na
virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha
kufanya tendo la ndoa.
0 comments: