Mazoezi ya mwili ni ya muhimu sana kwa afya yetu:
1. Mazoezi ya mwili husaidia kulirekebisha shinikizo la damu.
2. Mazoezi ya mwili huiruhusu damu nyingi zaidi kuzifikia sehemu zote za mwili na kuifanya mikono na miguu ipate joto.
3. Mazoezi ya mwili yanaondoa mambo yote mawili. Yaani mkazo wa mwili na mfadhaiko wa moyo, na kukusiadia wewe kujisikia vizuri zaidi katika maisha yako. Mazoezi ya mwili kwa kawaida ni tiba bora kabisa ya wasiwasi na msongo (stress).
4. Mazoezi ya mwili hutupatia nguvu ya umeme kwa ajili ya ubongo wetu pamoja na seli za neva. Yanaongeza afya kwa kuuamsha mfumo wa kinga mwilini (immune system).
Mwili unapowekwa katika hali ya afya kwa kufanya mazoezi yanayofaa. Ubongo unakuwa na uwezo wa kufikiri kwa ubunifu na ufanisi zaidi.
5. Yanaweza kukusaidia kuiweka vizuri rangi ya uso wako na kukuweka katika hali nzuri kabisa kimwili.
6. Mazoezi ya mwili hukufanya uwe na nguvu nyingi zaidi, hivyo kuchelewesha kupatwa na uchovu kimwili na kimawazo
7. Yanausaidia ubongo wako kutengeneza dawa inayokupa wewe hali ya kujisikia vizuri na kukuongezea uwezo wa kustahimili maumivu.
Endapo wewe ulikuwa hufanyi mazoezi, basi anza taratibu (polepole) na kuongeza nguvu yake hatua kwa hatua upatapo uwezo wa kustahimili. Laweza kuwa ni jambo la busara kumwona mganga wako kabla ya kuanza mazoezi hayo.
Lengo lako na liwe kujishughulisha na kila aina ya mazoezi hayo ya mwili ambayo yanaweza kulinganishwa na kutembea maili moja kwa dakika kumi na tano mara nne au zaidi kwajuma.
0 comments: