Chunusi
hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega na mgongoni kwa sababu maeneo hayo yana
vifuko au glandi za Sebaceous nyingi.
CHANZO
CHA CHUNUSI
Chanzo
halisi cha chunusi hakijulikani hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza
uwezekanifu wa kupata chunusi ni;
1. UMRI – Kama nilivyosema
hor-mone/vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa
kubale-he.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa nta (sebum) katika ngozi
ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
2. VIPODOZI –Baadhi ya vipodozi kama
Make-up za kina dada na Sprays za ny-wele zina mafuta ambayo yanaweza
kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
3. CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na
chakula bali baadhi ya vyakula hufan-ya chunusi kuwa nyingi zaidi.
4. DAWA- Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana
na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa
mpango,steroids na tranquilizers.Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa
kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na ma-kusudio ili
kuongeza unene wa misuli yao.
5. MAGONJWA- Magonjwa yatokanayo na
matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi
hasa kwa wasichana.
6. MAZINGIRA- Chunusi huweza kuwa nyingi
zaidi hasa unapoishi mazingira yenye mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho
sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.
7. JINSIA-Wavulana hupata sana
chunusi kuliko wasichana.
8. FAMILIA- Wakati mwingine chunusi
hujitokeza sana kwa wanafamilia wa familia kadhaa kuliko nyingine.
9. HOMONI- Mabadiliko ya homoni za
mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke
anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
10.
USAFI WA MWILI-
Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au
vipele hu-sababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwi-lini
au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi
Kesho
nitawaletea Matibabu ya chunusi…
0 comments: