1- Mpenzi/rafiki wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo asaidie au atoe.
2 - Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili.
3
- Ni
yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatojali umeongea
baya au zuri .
4 - Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuacha mtu wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.
5 – Mpenzi/rafiki wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa nyuma na kukuacha bila msaada .
6 – Mpenzi/rafiki wa kweli ni yule atakayekupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani (pesa au mali)
7 – Mpenzi/rafiki wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine
8 - Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli .
9 - Mpenzi/rafiki wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya maamuzi magumu .
10 - Atakuwa tayari kuvumilia hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu au ubabe. Ni hayo tu jipeme na umpime umpendaye!

0 comments: