Kumekuwa na malalamiko mengi baada ya
wajumbe wa katiba kutaka kuongeza posho zao ambazo hapo awali zilikuwa ni laki
3 kwa siku na sasa wanataka kuongeza mpaka laki 7 kwa siku kwa pesa za
kitanzania.
Hili swala limeleta mtafaruku mkubwa
kati ya wananchi na wabunge hao wanaotaka kutumia vibaya hela za walipa kodi.
Wafanya biashara wa Guest House walijua
neema itawashukia kwa wingi wa wajumbe hao kuja Dodoma lakini mambo
yamebadilika wateja ni wachache na hawajui wajumbe hao wanalala wapi kwa wingi
wao huo.
Wanasingizia gharama ya maisha Dodoma ipo
juu kulingana na mikoa mingine lakini wajumbe hao wachachi wao wapo kwenye
guest za gharama hapa Dodoma na wangine wengi wamepanga nyumba nzima na kuishi
humo watu zaidi ya 20 kwa kutandika magodoro chini wakati wa kulala.
Angalia maigizo haya kipato cha
mtanzania wa kawaida kwa mwaka ni laki 7 lakini wajumbe wa katiba wanataka laki
7 tena kwa siku wakati kwa sisi walala hoi hiyo ndiyo ya kipato cha mwaka
mzima.
Mshahara wa nesi kwa mwezi ni laki 2
ambaye analinda uhai wa wajumbe hao wanataka kujiongezea posho ila madakitari
kuongezwa posho zao mpaka wagome na kuandamana mtaani lakini bado wangine watafukuzwa
kazi kwa kudai ongezeko la mshahara.
Posho ya wajumbe wa katiba kwa siku ni
Mshahara wa mwalimu kwa mwezi na kama
wakiongezewa posho na kufikia laki 7 inamaana itakuwa mara mbili ya mshahara wa
mwalimu ambaye aliyempa elimu.
Hii ndio Tanzania…… Chukua chako mapema………
0 comments: