Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Kipindi cha kubalehe kwa Wasichana ni wakati wa mabadiliko makubwa katika mwili... Soma hapa zaidi upate kujua..




Kipindi cha kubalehe ni wakati wa mabadiliko makubwa. Mabadiliko mengine yataonekana wazi. Kwa mfano, homoni zitasababisha nywele ziote kwenye maeneo ya viungo vyako vya uzazi. Pia, matiti, kiuno, mapaja, na makalio yatakuwa makubwa. 

Mwili wako utaanza kubadilika na kuchukua umbo la mwanamke mkomavu. Usiwe na wasiwasi. Hupaswi kushangazwa mabadiliko hayo ni mambo ya kawaida kabisa. Na yanaonyesha kwamba mwili wako unajitayarisha kwa ajili ya wakati ambapo utaweza kupata mtoto!



Muda fulani baada ya kuanza kubalehe, utaanza kupata hedhi. Usipojitayarisha vya kutosha, badiliko hilo kubwa maishani mwako linaweza kuogopesha. Niliogopa sana nilipofikiria kwamba kwa miaka mingi nitakuwa nikipata hedhi kila mwezi!

Hata hivyo, kumbuka kwamba kupata hedhi kunaonyesha kwamba nguvu zako za uzazi zinakua. Ijapokuwa miaka mingi itapita kabla hujawa mzazi, unaendelea kukomaa na kuwa mwanamke. Vyovyote vile, kuanza kupata hedhi kunaweza kuwa jambo la kuhangaisha. 

Jambo kubwa zaidi ni kukabili ni kubadilika-badilika kwa hisia, Utafadhaika sana kwa kuwa hukujua kwa nini ungeweza kuwa na furaha mchana kutwa, na kulia kwelikweli usiku wa siku hiyohiyo.

Ikiwa hivyo ndivyo unavyohisi sasa, uwe na subira. Baada ya muda utazoea. kumbuka wakati unapofikia hatua ya kukubali kwamba ili uwe mwanamke mkomavu mabadiliko hayo lazima yatokee na umepewa zawadi ya uzazi. 

Inachukua muda kukubali jambo hilo na inakuwa vigumu sana kwa wasichana fulani lakini baada ya muda unajifunza kukubali mabadiliko hayo.

0 comments: