Siri Ya Mafanikio

Siri Ya Mafanikio
WASILIANA NASI KWA KUTOA USHAURI, MAFUNZO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA KUFICHUA SIRI YA MAFANIKIO KUPITIA Email; siriyamafanikio@gmail.com Au Phone; 0766912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII 0766 912725

BIASHARA YA KUKU, BATA, VIFARANGA NA MAYAI KWA ODA PIGA NAMBA HII  0766 912725
Images

Pata kujua Dalili za kubalehe kwa Kijana wa kiume…!!! Ungana nami kwa kusoma hapa….




Ikiwa wewe ni mvulana, kipindi cha kubalehe kitabadili sana sura yako. Kwa mfano, huenda mara nyingi ngozi yako ikawa na mafuta mengi na kutokeza chunusi. Inafadhaisha na kuvunja moyo sana kuwa na chunusi,  kupigana vita vikali na chunusi hizo. Huwezi kujua ikiwa zitakwisha au zitaacha makovu au ikiwa watu watakudharau kwa sababu una chunusi.



Kwa upande mwingine, huenda ukaona kwamba unazidi kuwa mkubwa na mwenye nguvu na kwamba mabega yako yanaanza kupanuka. Pia, wakati wa kubalehe, nywele zinaweza kuota kwenye miguu, kifua, na uso wako, na pia kwenye makwapa yako. Hata hivyo, kumbuka kwamba kuwa na nywele nyingi hakumaanishi kwamba wewe ni dume sasa; hilo ni jambo linalotegemea urithi tu.
Kwa kuwa sehemu mbalimbali za mwili wako hukua kwa viwango tofauti, unaweza kuhisi kwamba sura yako haipendezi. 

Katika miaka ya katikati ya utineja sauti yako inakuwa nzito zaidi hatua kwa hatua. Kwa muda fulani, sauti nzito inaweza kukatizwa-katizwa na sauti nyembamba na kali, jambo ambalo linaweza kukufanya uaibike. Hata hivyo, usijali. Baada ya muda, sauti yako itasawazika. Kwa sasa, kujifunza kutohangaishwa na hali hiyo kutakupunguzia aibu.

Mfumo wako wa uzazi unapozidi kukomaa, viungo vyako vya uzazi vitakuwa vikubwa na nywele zitaota kandokando. Pia vitaanza kutokeza umajimaji unaoitwa .begu. Umajimaji huo huwa na mamilioni ya mbegu za uzazi zisizoweza kuonekana kwa macho, ambazo hupitishwa wakati wa ngono. Mbegu moja inaweza kutungisha mimba yai la mwanamke na kutokeza mtoto.

Umajimaji huo unapoongezeka mwilini, kiasi fulani hufyonzwa mwilini, lakini mara kwa mara, mwingine unatoka usiku unapolala. Hilo ni jambo la kawaida.

Kushughulika na Mabadiliko ya Kihisia
Mfumo wa uzazi unapoendelea kukomaa, wavulana na wasichana huanza kuvutiwa na watu wa jinsia tofauti. Hata hivyo, kwa sasa unapaswa kutambua kwamba unahitaji kujifunza kuzuia tamaa zako za ngono. 

Kuna hisia nyingine pia ambazo hutokea katika kipindi cha kubalehe. Kwa mfano, huenda ukajiona kuwa mtu asiyefaa kitu. Vijana wengi huwa wapweke na kushuka moyo mara kwa mara. 

Ukweli ni kwamba: Hakuna njia yoyote salama ya kuharakisha au kukawiza jinsi mwili unavyokua. Kwa hiyo, badala ya kuchukia na kuogopa mabadiliko hayo, jipe moyo na usihangaishwe na mambo kupita kiasi. Kubalehe si ugonjwa, wala wewe si mtu wa kwanza kubalehe. Uwe na hakika kabisa kwamba maisha yako hayako hatarini hata kidogo. Dhoruba ya kubalehe itakapokuwa imepita, utaibuka ukiwa mtu mzima aliyekomaa!

JE, WAJUA . . . ?
Kipindi cha kubalehe chaweza kuanza mapema sana, kuanzia umri wa miaka minane hivi, au kinaweza kuchelewa na kuanza mtu anapokuwa katika miaka ya katikati ya utineja. Hata mtu aanze kubalehe wakati gani, haimaanishi kwamba ana kasoro.

Kuna hali nyingi zenye kutia wasiwasi katika kipindi cha kubalehe, na huenda usijue jinsi mwili wako utakavyokuwa siku inayofuata. Lakini kadiri unavyokua, unajifunza kukubali mabadiliko hayo na hata kuyafurahia.

0 comments: