Ukweli ni kwamba biashara yeyote inaweza kufanikiwa ikiwa itapata wateja
wengi wakutosha. Hivyo suala la msingi, sio biashara gani ya muhimu, bali ni
vigezo gani vya msingi ni kama vifuatavyo;
• Chunguza siri za biashara zinazofanikiwa na mifumo iliyopo nyuma yake.
Jaribu kuziangalia biashara za Wahindi na Waarabu zinazofanywa. Watu wengi huwa
na wazo la bidhaa ya kuuza au hata kutengeneza kama vile mshumaa, rangi,
shampoo nk lakini mara nyingi huwa hawana ujuzi wa kutengeneza mfumo mzuri wa
uletaji wa faida.
• Pata mlezi au mshauri
atakayekusaidia katika safari ya ujasiriamali. Neno mentor linamaanisha mtu
ambaye amefanikiwa kwenye jambo fulani na ana uwezo wa kuwasaidia/kuwaelekeza
watu wengine wafanikiwe kama yeye.
• Fanya kazi kwenye biashara ya
mtu aliyefanikiwa na ambaye unataka kuja kuwa kama yeye. Wakati mwingine, njia
ya mkato ya kujifunza biashara ni kukubali kutumika chini ya mtu mwingine ili
ujionee moja kwa moja uendeshaji wa biashara kabla hujaamua kuingia moja kwa
moja.
• Jenga tabia ya kuwauliza maswali
ya msingi wajasiriamali waliofanikiwa. Kila unapopata nafasi ya kuwa na mtu
tajiri, jipe moyo mara kwa mara halafu uliza swali hili: “Je siri ya mafanikio
yako ni nini?”Utashangaa jinsi ambavyo watu wengi si wachoyo wa siri zao za
mafanikio ili mradi tu uulize katika mazingira mazuri yenye heshima na hekima.
. Jijengee uwezo wa kuuza. Uwezo wa kuwashawishi watu waweze kununua
bidhaa yako au kutumia huduma yako ndiyo uweze kusimama katika ujasiriamali.
0 comments: